Umoja wa Mataifa unaendelea kufuatilia kwa karibu hali inayotia hofu kubwa Kaskazini Magharibi mwa Syria kufuatia taarifa kwamba askari kadhaa wa Uturuki wameuawa kwenye shambulio la anga. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerejelea wito wake wa kusitisha uhasama mara moja na kuokoa Maisha ya raia walio hatarini kufiuatia machafuko yanayoendelea na mashambulizi.
Zaidi ya watu 6000 nchini Chad, wakwiemo wanaume, wanawake na watoto wamekimbilia katika mji wa Tina na Karnoi huko Kaskazini mwa Darfur Sudan kutokana na mapigano kati ya makundi tofauti ya kabila la Zaghawa katika eneo la Tina, upande wa pili wa mpaka nchini Chad, imeeleza taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyochapishwa hii leo.
Wakati janga la kibinadamu likishuhudiwa nchini Burkina Faso, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema ongezeko katika mashambulizi linasababisha raia kukimbia kuelekea maeneo ya kusini karibu na Mali na Niger.
“Hakuna suluhu ya kijeshi kwenye mzozo wa Syria,” amesisitiza tena hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres huku akitoa wito kwa kumalizwa kwa janga hilo lililosababishwa na binadamu na kuleta machungu ya muda mrefu kwa wananchi wa Syria.
Takribani watu milioni 6.5 nchini Sudan Kusini, ambao ni zaidi ya nusu ya watu wote wa Sudan Kusini, wanaweza kuwa hatarini kukumbwa na baa la njaa katika miezi ya Mei na Julai, yameonya mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa.
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo wamejulishwa kuwa mwaka huu wa 2020 utakuwa mwaka muhimu sana na wa kihistoria kwa wananchi na taifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.
Nchini Niger, takribani watu milioni 3 wanahitaji, zaidi ya nusu yao wakiwa ni watoto,wanahitaji msaada wa kibinadamu wakati huu ambapo taifa hilo linakabiliwa na ukosefu wa usalama, utapiamlo, magonjwa, mafuriko na ukimbizi wa ndani.
Taarifa iliyotolewa hii leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura OCHA, imenukuu ripoti za kuaminika zisemazo kuwa mnamo tarehe 14 mwezi huu wa Februari, watu wenye kujihami kwa silaha waliwaua raia 20 wakiwemo watoto katika Kijiji cha Ntumbo, eneo la Kaskazini Magharibi mwa Cameroon.
Itakuwa gharama ndogo kwa sasa kulisaidia shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO kupambana na nzige Afrika Mashariki kuliko kuwasaidia mamilioni ya watu katika ukanda huo baada ya mazao yao yote kusambaratishwa, ameonya mkurugenzi mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP David Beasley.
Mvua kubwa zilizonyesha kwa wiki mbili zilizopita nchini Madagascar zimeathiri watu 120,000 ikiwakata kabisa na huduma za barabara, kusambaratisha shule 174, na kuwalazimisha watu 16,000 kusalia bila makazi.