Msaada wa Kibinadamu

Wakimbizi 25,000 kutoka Eritrea wapokea msaada jimboni Tigray Ethiopia:UN

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamefikisha msaada wa chakula wa kuokoa Maisha kwa wakimbizi 25,000 kutoka Eritrea walioko kwenye jimbo la Tigray nchini Ethiopia. 

Ongezeko la machafuko CAR linatia hofu kubwa: OCHA 

Mapigano na mivutano iliyoshuhudiwa wiki iliyopita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, ina athari kubwa kwa ulinzi wa raia nchini humo limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA. 

UNICEF yaingilia kati kuokoa watoto Korogocho Kenya 

Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kwa msaada wa shirika la Uingereza, UK Aid, linasaidia kutoa huduma ya ulinzi kwa watoto katika makazi  duni au yasiyo rasmi, Korogocho, walioathiriwa na kufungwa kwa shule kutokana na janga la COVID-19.

Dola milioni 156 zahitajika kusaidia wanaokimbia ghasia Tigray- UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR pamoja na wadau 30 wa kibinadamu  hii leo wanatoa wito wa dharura kupatiwa wa dola milioni 156.
 

Ni maafa mazito, tuna njaa, asema mkimbizi wa Syria aliyeko Lebanon. UNHCR inajitahidi kusaidia. 

Ripoti hiyo ya Benki ya Dunia na UNHCR imechunguza madhara ya ugonjwa wa COVID-19 katika kuwasukuma wakimbizi wa Syria katika umaskini, wao pamoja na wenyeji wao nchini Jordan, Lebaon na aneo la Kurd nchini Iraq.  

Hali bado ni tete kwa watoto Cabo Delgado

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema takribani watoto 250,000 wamekimbia makazi yao kutokana na ghasia zinazoendelea kwenye jimbo la Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji na sasa wako hatarini kupata magonwa ya kuambukiza kwa kuwa msimu wa mvua unaanza.

UNICEF yatoa msaada wa dharura wa chakula kwa watoto nchini Uingereza

Maelfu ya familia zilizoathirika na janga la corona au COVID-19 nchini Uingereza zitapokea msaada wa dharura wa chakula kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika kipindi cha sikukuu na zaidi limetangaza shirika hilo likiongeza kuwa msaada huo utakuwa ni wa mara moja tu. 

WFP yaonya kuhusu upungufu wa chakula kwa ajili ya wakimbizi Kenya

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP leo limeonya kuwa zaidi ya wakimbizi 435,000 nchini Kenya wanakabiliwa na uhaba wa chakula iwapo hautapatikana ufadhili wa dola milioni 57 kuendelea kutoa chakula Dadaab, Kakuma na Kalobeyei. 

Msaada wa nchi tajiri kwa watoto wakati wa COVID-19 hautoshi:UN Ripoti 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limekosoa kiwango cha msaada wa kifedha uliotengwa kwa ajili ya kusaidia watoto katika nchi tajiri wakati huu wa janga la corona au COVID-19 na kusema hakitoshi. 

WFP yaendelea kutoa chakula kwa wakimbizi wanaovuka kuingia Sudan wakitokea Tigray  

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP, hii leo mjini Geneva Uswisi limeeleza kuwa  hadi kufikia sasa limeweka vituo sita vya usambazaji wa uhifadhi wa chakula na misaada mingine muhimu ya kibinadamu kwa wakimbizi wanapohamia katika kambi mbalimbali nchini Sudan.