Msaada wa Kibinadamu

Hali wanayoishi Watoto Rukban haikubalika katika karne ya sasa-UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema watoto katika makazi ya muda ya Rukban kusini mwa Syria mpakani na Jordan wanaishi katika hali mbaya isiyokubalika katika karne hii ya 21.

 

Msafara mkubwa kabisa wa msaada wa kibinadamu wawafikia maelfu Rukban:UN

Umoja wa Mataifa na chama cha msalama mwekundu nchini Syria leo wamekamilisha zoezi la kupeleka misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi wa ndani zaidi ya 40,000 kwenye kambi ya Cyclone Kusini mwa Syria katika msafara na operesheni ambayo ni kubwa kabisa kuwahi kufanywa na Umoja wa Mataifa nchini humo.

Bila rasilimali za kutosha WFP haiwezi kufikia watoto ambao maisha yao yako hatarini Yemen

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema licha ya mpango wake wa dharura wa kusambaza chakula nchini Yemen kuwa mkubwa zaidi kuliko yote duniani ukilenga kila mwezi kuwalisha watu milioni 12 wenye njaa kali na walioko hatarini zaidi, bado takribani watu milioni 16 nchini humo wanahaha kupata mlo kila siku kutokana na uhaba wa chakula. 

FAO yachukua hatua kupunguza makali ya El Nino kwa wakulima na wafugaji Malawi

Shirika la chakula na kilimo duniani,  FAO kwa usaidizi wa Belgium limeandaa mradi wa kupunguza makali ya madhara ya ukame uliosababishwa na El Nino nchini Malawi mwaka jana wa 2018.

Jamani jiungeni nasi kwenye mradi wa kuondoa umaskini CAR- Mnufaika

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu, CAR, kwa kushirikiana na wadau wameanzisha mradi wa kuwajengea uwezo wapiganaji waliosalimisha silaha zao na kuwa raia wema.

 DRC ni kimbilio kwa maelfu ya watu wanaokimbia machafuko Sudan Kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema limeshuhudia ongezeko la wakimbizi kutoka nchini Sudan Kusini wanaowasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,DRC.

Vietnam yatoa msaada kwa dola 50,000 kusaidia shughuli za WFP huko Cox’s Bazar.

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP leo limekaribisha mchango mpya wa dola 50,000 kutoka Vietnam kwa ajili ya shughuli za mpango huo katika kambi za wakimbizi wa Rohingya huko Cox’s Bazar nchini Bangladesh.

Dola milioni 43.5 zinahitajika mwaka huu kuimarisha huduma za afya Libya- WHO

Shirika la afya duniani WHO na washirika wake wametangaza ombi la dola milioni 43.5 ili kuimarisha huduma za afya nchini Libya hususan kwa watu 388,000 walioathirika na mgogoro unaoendelea nchini humo.

Shehena ya chakula cha msaada Yemen iko hatarini kuoza- UN

Umoja wa Mataifa umesema suala la la kuyafikia maghala ya shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, yaliyohifadhi shehena ya nafaka huko Hudaidah nchini Yemen linazidi kupata umuhimu zaidi kila uchao.

Viongozi wa Afrika wanusuruni watoto milioni 13.5 waliofurushwa makwao– UNICEF

Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Muungano wa Afrika, AU ukianza kesho Jumamosi huko Addis Ababa Ethiopia, takribani Watoto milioni 13.5 barani Afrika wamefurushwa makwao.