Msaada wa Kibinadamu

Mlo wa siku moja tu ni changamoto kwa wakimbizi na wasaka hifadhi Misri.

Shirika  la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR hii leo mjini Geneva Uswisi limesema msaada unaotolewa kwa wakimbizi walioko Misri uko katika wakati mgumu kutokana na kuongezeka kwa wakimbizi wapya huku kukiwa na vyanzo haba vya rasilimali.

WFP yasafirisha vyakula kwa njia ya anga kwenda kuokoa maisha Zemio, Afrika ya kati.

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP hii leo limetangaza kuzindua operesheni ya kusafirisha chakula kwa kutumia ndege ili kuokoa maisha ya watu 18,000 katika eneo la Zemio takribani kilomita 1000 mashariki mwa mji mkuu wa Afrika ya kati, Bangui. 

WFP yaweza kufikia kinu cha kusagisha nafaka cha Red Sea

Hatimaye shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limepata fursa kwa mara ya kwanza kabisa tangu mwezi Septemba mwaka jana kufikia kinu cha kusagisha nafaka cha Red Sea nchini Yemen.

Wazee nchini Mali washukuru mola kwa jinsi operesheni FADEN 6 inavyogusa maisha yao.

Nchini Mali operesheni FADEN-6 ya ujumbe wa Umoja wa  Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo, MINUSMA umeleta matumaini kwa jamii hususan zile ambazo hazikuwa na matumaini ya kupata siyo tu matibabu bali pia maridhiano baina yao. 

Dola bilioni 2.6 zaahidiwa kuinusuru Yemen:UN

Wahisani waliokusanyika mjini Geneva  Uswisi hii leo wameahidi dola bilioni 2.6 ili kuhakikisha kwamba operesheni za misaada ya kibinadamu zinaendelea nchini Yemen katika wakati huu ambao msaada ndio tumaini pekee la mamilioni ya Wayemen. 

Bila fedha mamilioni ya walio na njaa Yemen watakuwa njia panda:WFP

Wakati mkutano wa kimataifa wa uchangishaji fedha kwa ajili ya Yemen ukifanyika leo mjini Geneva Uswis na kuwaleta pamoja wadau mbalimbali  wa kimataifa na mashirika wahisani, shirika la Umoja wa  Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, limesema linahitaji haraka dola milioni 570 ili kususuru maisha ya mamilioni ya wanaohitaji msaada wa chakula. 

Mamlaka Venezuela msitumie silaha za sumu dhidi ya waandamanaji- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo amekuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, Jorge Arreaza, ambapo amesisitiza tena kuwa hatua zozote ambazo chombo hicho kitachukua kusaidia wahitaji nchini Venezuela zitazingatia kanuni na misingi ya kibinadamu, kutoegemea upande wowote na mamlaka za taifa hilo na kushirikiana na taasisi za taifa hilo.
 

Dhamira ipo katika kutekeleza makubaliano ya Stockholm, Yemen-Griffiths

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen, Martin Griffiths leo amehutubia kikao cha Baraza la Usalama kwa njia ya video kuhusu kile alitaja kama hatua chanya katika utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa mjini Stockholm nchini Sweden.

Hali ya kisiasa Burundi yatia matumaini- Kafando

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Burundi, Michel Kafando amesema hali ya kisiasa nchini humo imeanza kutia matumaini wakati huu ambapo taifa hilo linajiandaa kufanya uchaguzi mkuu hapo mwakani.

UN-Habitat kupata dola laki 7 kutoka Japan kusaidia wanaorejea Darfur Kusini, Sudan.

Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT mjini Khartoum nchini Sudan limetangaza kuwa Japan imeahidi mchango wa dola laki 7 kwa ajili ya mradi wa kusaidia wakimbizi wa ndani wanaorejea katika eneo la Alsalam, Darfur kusini nchini humo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Machi  mwaka huu hadi Machi mwakani.