Nchini Somalia, katika jimbo la Puntland, harakati za kujikwamua dhidi ya ukame na njaa zinazidi kutia matumaini lakini bado hatua zaidi zahitajika ili wananchi wasitumbukie tena kwenye baa la njaa.
Ghasia zikishamiri huko jimbo la Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na ufikishaji misaada nao ukigonga mwamba, shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limeibuka na mbinu mpya za kukabili njaa.
Leo ni siku ya wapendao duniani , shirika la Umoja la idadi ya watu duniani UNFPA imetoa wito , tafadhali wakati unaadhimisha siku hii wakumbe wanaoingizwa katika ndoa za shuruti na kusema, imetosha, sasa ni marufuku.
Amkani si shwari tena kwenye jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako raia wanakimbia mapigano kati ya jamii ya wahemba na walendu. Safari sasa ni kuelekea Uganda kupitia ziwa Albert.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za ajali mbaya ya ndege iliyotokea leo karibu na mji mkuu wa Urusi Mosco ambapo abiria wote na wafanyakazi wa ndege waliokuwemo wamearifiwa kupoteza maisha.
Shirika la Umoja w aMataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), limeripoti kuwa wakimbizi takribani 4,000 wamekimbilia Uganda kufuatia kushamiri kwa mzozo wa kikabila Jimbo la Ituri na mashambulizi ya vikundi vilivyojihami Jimboni Kivu Kaskazini katika kipindi cha wiki moja tu.
Wakati vita na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi vikiendelea kupandisha idadi ya wanaokabiliwa na njaa duniani baada ya idadi hiyo kupungua kwa miongo, sasa shirika la chakula na kilimo FAO linahitaji zaidi ya dola bilioni moja ili kuokoa maisha na kushughulikia tatizo la njaa kwa nchi 26.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lile la mpango wa chakula, WFP na lile la chakula na kilimo FAO na ofisi ya usaidizi wa dharura, OCHA yamesema kwamba ukosefu wa nvua mwishoni mwa mwaka 2017 na mwanzoni mwa mwaka huu wa 2018 unahatarisha uzalishaji wa chakula kwa nchi za kusini mwa Afrika.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limeonya kwamba msimu wa pepo kali na mvua za monsoon utawaweka hatarini maelfu ya wakimbizi wa Rohingya walioko Bangladesh na hivyo likishirikiana na wadau wengine wanajiandaa kukabiliana na athari zake.