Raia wa Venezuela 117,000 wameomba hifadhi mwaka huu hadi kufikia sasa, ikiwa ni idadi kubwa kuliko raia wote wa nchi hiyo walioomba hifadhi kwa mwaka mzima wa 2017 limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, baada ya uamuzi wa mahakama kuu ya Brazil kutengua uamuzi wa jaji wa jimbo kufunga mpaka wa Kaskazini unaopakana na Venezuela.