Kamishina mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya wakimbizi Filippo Grandi, ametoa wito kwa matifa wahisani kusaidia kurejesha utulivu katika nchi za Afrika zilizoghubikwa na migogoro.
Kuendelea kushika kasi kwa msimu wa pepo kali na mvua za monsoon kumeongeza shinikizo la mahitaji ya kiafya kwamaelfuya wakimbiz wa Rohingya walioanza kumiminika nchini Bangladesh kwa wingi yapata miezi 10 iliyopita.
Wiki moja baada ya mapigano kuanza kwenye uwanja wa ndege katika mji wa bandari wa Hodeidah, maelfu ya raia wamesalia katika hatari kubwa hali ambayo inalitia hofu kubwa shirikala Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA.
Kuendelea kwa mapigano mjini Hudaidah nchini Yemen kunahatarisha wakazi ambao ni waathirika wa moja kwa moja na asilimia 70 ya watu wanaotegemea huduma muhimu ikiwemo, huduma ya afya inayopita bandari iliyomo mjini humo.
Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO, limeanza kuwajengea uwezo wataalamu wa kuandaa mipango ya kukabili maafa nchini Tanzania kama njia mojawapo ya kupunguza maafa.
Watoto milioni 1.6 wanakabiliwa na utapiamlo uliokithiri katika mataifa sita ya eneo la Sahel barani Afrika na hivyo kunahitajika msaada wa haraka kuweza kubadilisha hali hiyo.
Pepo za monsuni huko barani Asia zimeanza kuonyesha uharibifu wake hususan kwa wakimbizi wa Rohingya walioko kwenye kambi ya Cox’s Bazar nchini Bangladesh.