Hali ya usalama na kibinadamu ikiendelea kuzorota nchini Yemen, hususan mji wa bandari wa Hodeidah, WHO imechukua hatua ili kuhakikisha huduma za afya zinaimarika.
Nchini Yemen kuna nuru sasa ya mazungumzo kati ya pande kinzani. Umoja wa Mataifa umeelezea matumaini hayo wakati huu ambapo tayari chombo hicho kimeruhusiwa kusimamia bandari muhmu ya Hodeidah.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesihi Muungano wa Ulaya, EU, na wanachama wake kuchukua hatua thabiti, za pamoja na za wakati il kuokoa Maisha ya watoto wakimbizi na wahamiaji kabla hawajaingia barani Ulaya.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ana wasiwasi mkubwa kutokana na matukio ya mara kwa mara ya mapigano kati ya wakulima na wafugaji wanaohamahama kwenye maeneo ya Afrika Magharibi na Kati.
Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na UKIMWI -UNAIDS, umekaribisha mchango wa nyongeza wa zaidi ya dola 977,000 kwa ajili ya harakati zake za kupambana na ugonjwa huo.
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo wamejulishwa kuwa hali ya usalama na kibinadamu nchini Syria inazidi kudorora kutokana na mashambulizi yanayoendelea hivi sasa dhidi ya raia hususan kusini mwa nchi hiyo.
Baada ya miezi kadhaa ya kujaza udongo na kunyanyua maeneo ya ardhi ili kuwa na eneo tambarare, hatimaye baadhi ya wakimbizi warohingya huko Bangladesh sasa wana amani kwani ujio wa mvua za pepo za monsuni sasa si tishio tena kwa uhai wao.