Msaada wa Kibinadamu

Heko G5 huko Sahel kwa kulinda raia-UN

Ukanda wa Sahel unakabiliwa na mashambulizi na shida za mara kwa mara ambapo nchi tano kwenye ukanda huo zimeunda kikosi cha kukabili mashambulizi kiitwacho, G5.

Hungary tupilieni mbali mswada wa sheria zitakayowaathiri wakimbizi: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limetoa wito kwa serikali ya Hungary kuachana na mswada wa sheria zinazotarajia kuwasilishwa bungeni ambazo zitabana uwezo wa mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s na watu binafsi kuwasaidia waomba hifadhi na wakimbizi.

IOM yasaidia kuwarejesha Ethiopia wahamiaji 100 Kutoka Yemen

Raia 101 wa Ethiopia waliokuwa wahamiaji nchini Yemen wameondoka kwa hiyari kwa msaada wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM na kurejea nyumbani kupitia bandari ya Hudaydah.

Watu milioni 1.9 CAR wahitaji msaada-OCHA

Jamhuri ya Afrika ya Kati-CAR,  inakabiliwa  na mgogoro mkubwa wa kibinadamu.  Mratibu wa masuala ya kibanadamu nchini humo amesema hali si shwari na usaidizi zaidi unahitajika ili kunasua wananchi walio taabani.

Hali ya kibinadamu si shwari Yemen : OCHA

Hali ya kibinadamu nchini Yemen inazidi kuzorota kutokana  kuongezeka kwa migogoro, vikwazo dhidi ya misaada ya kibinadamu na kupungua kwa uingizaji wa biashara muhimu hivyo kusababishwa mamilioni ya waYemen kukabiliwa  uhaba mkubwa wa chakula.

Juhudi dhidi ya Ebola DRC zijumuishe watoto- UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetaka harakati za kukabiliana na mlipuko wa Ebola huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ujumuishe watoto.

WHO na Benki ya Dunia waunda bodi kudhibiti milipuko ya magonjwa

 

Shirika la Afya ulimwenguni WHO na Benki ya dunia wameunganisha jitihada zao na kuunda bodi itakayosaidia kuimarisha usalama wa afya duniani.

Priyanka apaza sauti za watoto warohingya

Balozi mwema wa UNICEF, Priyanka Chopra amezuru kambi ya wakimbizi wa Rohingya huko Bangladesh na kutoa wito kwa usaidizi zaidi kwa watoto wa wakimbizi hao ambao maisha yao yako taabani.

Madhara ya ukimwi yagharimu mabilioni ya fedha- ILO

 

Ugonjwa wa Ukimwi pamoja na kusababisha machungu kwa binadamu, pia husababisha kupotea kwa mabilioni ya mapato ya fedha kutokana na vifo vya mamia ya maelfu ya wafanyakazi ambavyo vinaweza kuzuilika kwa matibabu.

 

Ulinzi wa raia vitani- maneno mengi kuliko vitendo

Mizozo kote duniani inaibua vitisho na machungu kwa mamilioni ya raia wakiwemo wanawake, wasichana, wanaume, wavulana na watoto.