Wakati serikali ya Iraq ikiibuka kutoka kwenye machafuko ya miaka minne, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP ,limepokea dola milioni 10 kama mchango wa serikali ya Japan kusaidia ujenzi mpya Iraq.
Idadi kubwa ya wakimbizi wa Burundi wanahofiwa kufariki dunia baada ya mabasi walimokuwa wakisafiria kurejea nyumbani kutoka Tanzania kupata ajali mkoani Kagera, kaskazini-magharibi mwa Tanzania.
Mkutano na waandishi wa habari, Guterres amulika zaidi mabadiliko ya tabianchi na hatua anazoamini kuwa zinapaswa kuchukuliwa. Azungumzia pia matarajio yake kuhusu kinachoendelea rasi ya Korea na mvutano kati ya Urusi na mataifa mengine duniani.
Maelfu ya wakimbizi wa Ethiopia wanaohifadhiwa nchini Kenya hivi sasa wanakabiliwa na mtihani mkubwa wa kukidhi mahitaji yao ya msingi kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.
Dola bilioni 2.7 kusaidia nchi za Sahel na kiwango hicho cha fedha kimetangazwa leo huko Mauritania na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J Mohamed .
Syria! Syria! Syria! Bado ni kizungumkuzi, maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanapitishwa lakini wahusika ni kama kusema "wameweka pamba masikioni."
Mizozo na njaa kali vyaendelea kuambatana kwenye maeneo kadhaa duniani na kuacha watoto, wanawake, wanaume, vijana kwa wazee hoi bin taaban. Baraza la Usalama lakumbushwa wajibu wake.