Msaada wa Kibinadamu

Msaada wa dharura wahitajika Somalia

Idara ya kuratibu huduma za dharura za UM, OCHA imeonya kwamba bila ya kuongezwa haraka msaada kukabiliana na janga kubwa la utapia mlo na magonjwa huko Somalia, basi hali hiyo itazidi kuzorota.

Tume ya UM yatoa mwito kuimarisha juhudi za huduma Zimbabwe

Tume maalum ya idara za UM huko Zimbabwe imesisitiza kwamba hali ya kibinadamu inaendelea kua mbaya sana na kuhimiza serekali na jumuia ya kimatiafa kusaidia kuimarisha juhudi za msaada wa dharura.

Qatar yatoa $ milioni 40 kwa ajili ya misaada ya dharura

Serekali ya Qatar imetangaza hii leo kwamba imetoa msaada wa dola milioni 40 ili kusaidia mipango ya huduma za dharura ya UM kote duniani.

UNRWA itaanzisha tena huduma zake Ghaza kufuatia kurudishwa kwa misaada iliotaifishwa

Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa KiFalastina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) limeripoti kwamba kundi la Hamas, lenye kushika madaraka kwenye eneo liliokaliwa la Tarafa ya Ghaza, limerudisha zile bidhaa za misaada ilioitaifishwa na wao wiki iliopita.

UNRWA yasimamisha, kwa muda, misaada ya kihali kwa Ghaza

Shirika la UM Linalofarajia WaFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA) limetoa taarifa yenye kusema wanasimamisha kuingia Tarafa ya Ghaza bidhaa zote za misaada, baada ya wenye madaraka kutaifisha mamia ya tani za msaada wa chakula mnamo usiku wa Alkhamisi ya tarehe 05 Februari (2009).

WHO kuipatia Kenya msaada wa tiba kwa waathirika wa ajali ya moto

WHO imetangaza kuipatia Kenya yuro 50,000 kusaidia kutibu waathirika wa moto uliotokana na tangi la mafuta ya petroli, ajali ilioua karibu watu 100.

WFP itaisaidia Kenya kumudu upungufu wa nafaka, madhara ya ukame na chakula ghali

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuwa wiki hii litatuma timu ya watathmini wataalamu, kukadiria mahitaji halisi ya chakula kwenye yale maeneo ya Kenya yanaosumbuliwa na upungufu wa mvua mnamo mwaka uliopita.

Wenye njaa Ghaza kuhudumiwa na WFP vyakula viliopikwa

Wagonjwa na majeruhi waliowekwa kwenye hospitali za eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza, wanatarajiwa kupokea misaada ya vyakula vilivyopikwa tayari, kutoka Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP), ili kuwanusuru na hatari ya njaa, kwa sababu ya upungufu wa chakula na nishati uliochochewa na mashambulizi ya karibuni ya Israel kwenye eneo hilo.

UNICEF inaomba ifadhiliwe dola milioni 34 kuhudumia waathirika wa mashambulio na uvamizi katika Ghaza

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Mendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetoa ombi liliopendekeza lifadhiliwe haraka mchango wa dharura wa kukidhi mahitaji ya kihali, kwa wale watoto na aila zao, ambao waliathirika hivi majuzi kutokana na mashambulio ya mabomu na vurugu lilioendelezwa na vikosi vya Israel kwenye Tarafa ya Ghaza.

UM umeanzisha kampeni ya kufufua huduma za kiuchumi na jamii Ghaza

Ijumatatu, mjini Geneva, John Holmes, Naibu KM juu ya Masuala ya Kiutu alianzisha rasmi kampeni ya kuchangisha msaada wa dola milioni 613, kutoka wahisani wa kimataifa, msaada unaohitajika kukidhi mahitaji ya kihali kwa waathirika wa mashambulizi ya karibuni ya vikosi vya Israel, yaliofanyika kwenye eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza.