Msaada wa Kibinadamu

Ujapani yafadhilia UNICEF msaada maalumu kuhudumia watoto wa Ghaza

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF) limepokea msaada wa dola milioni 3 hii leo kutoka serikali ya Ujapani, uliodhaminiwa kuwasaidia waathirika watoto Ghaza kufuatia mashambulio ya karibuni kwenye eneo hilo.~~~

Msaada wa Ujapani kwa Bonde la Ufa utatumiwa kufufua huduma za kijamii

Kadhalika, Serikali ya Ujapani imefadhilia dola milioni 7 leo hii, kutumiwa kwenye ile miradi ya kufufua huduma za kimsingi kwa maelfu ya wakazi wa eneo la Bonde la Ufa nchini Kenya, raia ambao waliathiriwa kihali na vurugu liliozuka nchini mwao, kufuatia uchaguzi uliopita. Jemini Pandya, Msemaji wa Shirika la Kimataifa juu ya Wahamaji (IOM) aliwaambia waandishi habari Geneva taarifa zaidi juu ya msaada huo:~

WFP kuongeza huduma za dharurua kwa umma wa Ghaza

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) leo limeanza kugawa kashata za rutubishi za tende pamoja na biskuti maalumu za kutia nguvu, kwa maelfu ya wakazi wa KiFalastina wanaoishi kwenye eneo liliokaliwa la Tarafa ya Ghaza, kufuatia wiki tatu ya mashambulio ya vikosi vya Israel.

Mratibu wa UM juu ya Misaada ya Kiutu azuru Ghaza

John Holmes, Mratibu wa UM juu ya Misaada ya Dharura na Masuala ya Kiutu ameanza ziara ya siku nne katika Israel na kwenye eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza, kwa makusudio ya kutathminia mahitaji hakika ya kihali kwa waathirika wa operesheni za karibuni za majeshi ya Israel kwenye eneo hilo.

WFP yasisitiza watumishi wake lazima wapewe ulinzi bora kuweza kuendelea na huduma za kunusuru maisha Usomali

Kwenye taarifa nyengine, kuhusu shughuli za Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP), tumearifiwa kwamba UM unazingatia kusimamisha, kwa muda, huduma zake katika Usomali mpaka pale itakapothibitishiwa hifadhi inayofaa, na ulinzi bora, kwa watumishi wake.

Hasara na vifo kutokana na maafa vilikithiri ulimwenguni katika 2008 - ISDR

Taasisi ya UM juu ya Kupunguza Maafa (ISDR)imeripoti kutoka Geneva kwamba mwaka 2008 ulishuhudia muongezeko mkubwa wa vifo na hasara za kiuchumi kutokana na maafa ya kimataifa, tukilinganisha na takwmiu wastani za kila mwaka kuhusu ajali hizo katika miaka ya 2000 hadi 2007.

UNICEF/WHO kufadhiliwa dola milioni 9.7 na Waqf wa Gates kuhudumia watoto dawa bora

Taarifa iliotolewa bia leo hii na mashirika mawili ya UM yanayohudumia maendeleo ya watoto, yaani UNICEF, na afya duniani, yaani WHO, imepongeza msaada wa dola milioni 9.7 waliopokea kutoka Waqf wa Bill na Melinda Gates, kwa makusudio ya kuimarisha utafiti wa kutengeneza dawa zitakazotumiwa makhsusi, na kwa urahisi, na watoto wadogo chini ya umri wa miaka kumi na tano.

Msemaji wa UNRWA akiri hali shwari Ghaza lakini bado ni ya wasiwasi

Chris Gunness, Msemaji wa Shirika la UM Linalofarajia Misaada ya Kihali kwa WaFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA) alihojiwa Ijumatatu, kwa kupitia njia ya simu, na Idhaa ya Redio ya UM-Geneva ambapo alielezea namna hali ilivyo sasa hivi katika Ghaza, baada ya kutangazwa vikosi vya Israel vinasimamisha mashambulizi:~

Ofisa wa UNRWA anasema hali Ghaza ni ya kutisha mno

John Ging, Mkurugenzi wa Operesheni za Shirika la UM la Kufarajia Wahamiaji wa KiFalastina kwenye Mashariki ya Karibu (UNRWA) ameiambia Ofisi ya UM, Geneva, hii leo, kwa kutumia njia yasimu, ya kwamba mipangilio ya kuhudumia misaada ya kihali Ghaza, kwa umma muhitaji, imevurugwa kwa sasa, kwa sababu ya kuendelea kwa mapigano, hali ambayo vile vile alisema imeongeza khofu na wasiwasi miongoni mwa wakazi wa Ghaza pamoja na umma wa eneo jirani.

Haki za binadamu zakiukwa Ghaza, inasema UM

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu baada ya majadiliano ya siku mbili, kwenye kikao cha dharura, Ijumatatu mjini Geneva limepitisha azimio lenye kulaani vikali operesheni za kijeshi zinazoendelea sasa hivi za vikosi vya Israel kwenye eneo liliokaliwa la WaFalastina la Ghaza.