Msaada wa Kibinadamu

Watu milioni 6.2 Ethiopia wanakabiliwa na hatari maututi ya utapiamlo, OCHA inahadharisha

Fidele Sarassoro, Mratibu wa Misaada ya Kiutu katika Ofisi ya UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) ametangaza kwamba taifa la Ethiopia linakabiliwa kwa sasa na tatizo la kuhudumia mamilioni ya raia misaada ya kihali, kwa sababu ya upungufu wa chakula, huduma za afya, lishe bora pamoja na maji safi na usafi wa mazingira, ikichanganyika pia na matatizo ya ukosefu wa makazi ya dharura, ajira na ukosefu wa shughuli za kilimo ambazo zinahitajika kuwasaidia raia kupata riziki.

Ethiopia kufadhiliwa msaada wa dharura na CERF

Taasisi ya Mfuko wa UM juu ya Maafa ya Dharura au Mfuko wa CERF, Alkhamisi imetangaza kutoka Geneva ya kuwa itaifadhilia Ethiopia msaada wa dola milioni 6,

EU inashirikiana na FAO kupiga vita njaa kwenye nchi maskini

Ripoti za UM zimethibitisha ya kuwa katika 2009 watu bilioni moja ziada husumbuliwa na upungufu wa chakula na njaa sugu katika dunia.

OCHA inasema inahitaji msaada wa bilioni $4.8 kukidhi mahitaji ya waathirika maafa ulimwenguni

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti leo ya kuwa kuna upungufu wa dola bilioni 4.8 za msaada wa fedha zinazotakikana, katika miezi sita ya mwanzo wa 2009, kukidhi mahitaji ya kiutu kwa watu walioathirika na maafa.

Raisi mstaafu wa Ghana ameteuliwa na WFP kusaidia kukomesha njaa inayosumbua watoto

Raisi mstaafu wa Ghana, John Kufuor, ameteuliwa rasmi na Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) kuwa Balozi Mtetezi mpya dhidi ya Njaa Duniani.

Waathirika wa uhasama katika JKK wafadhiliwa $7 milioni na Mfuko wa CERF kukidhi mahitaji ya kimsingi

Taasisi ya Mfuko wa UM juu ya Maafa ya Dharura au Mfuko wa CERF imetangaza ya kuwa itafadhilia msaada wa dola milioni 7, kukidhi mahitaji ya dharura kwa watu 250,000 waliopo kwenye majimbo yenye matatizo ya Kivu Kusini na Kaskazini.

OCHA inasema waasi wa Uganda wanaendelea kutesa raia katika JKK

Tawi la Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) iliopo Nairobi, Kenya limetoa taarifa yenye kuthibitisha waasi wa Uganda wa kundi la LRA, waliojificha kwenye maeneo ya kaskazini-mashariki, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) wanaendelea kuhujumu na kuteka nyara, pamoja na kuua raia wa katika eneo.

Hatua za dharura kwenye sekta ya afya zinahitajika Usomali kunusuru maisha ya waathirika wa mapigano na vurugu

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeeleza kwamba mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalioshtadi nchini Usomali kwa sasa hivi, yamesawijisha na kudhoofisha sana huduma za afya pamoja na miundombinu ya kijamii, hususan kwenye maeneo ya Kati na Kusini mwa nchi.

Wataalamu wa FAO wanaashiria Benin itajitosheleza mahitaji ya mpunga katika 2011

Wataalamu wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) wanaashiria taifa la Benin, katika Afrika Magharibi, kutokana na mradi mpya utakaowasilishwa nchini humo katika miezi ya karibuni, taifa hilo litaweza kuzalisha mavuno ya mpunga kwa kiwango kikubwa kabisa na kupunguza gharama za kuagiza mpunga kutoka nchi za kigeni.

Amani ya chakula ndio msingi wa usalama wa dunia:IFAD

Kanayo Nwanze, Raisi wa Taasisi ya UM juu ya Mfuko wa Kimataifa kwa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kwenye mahojiano aliofanya na Redio ya UM alisisitiza juu ya umuhimu wa ile rai ya walimwengu kuhakikisha kunakuwepo akiba maridhawa ya chakula duniani.