Msaada wa Kibinadamu

WFP inayashukuru mataifa kwa kusaidia kuhudumia chakula wenye njaa katika 2009

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) leo limetoa taarifa maalumu, ya shukurani, kwa Mataifa Wanachama katika sehemu zote za dunia, kwa kazi ngumu na misaada waliochangisha katika zile huduma za kupiga vita njaa ulimwenguni mnamo 2009.

Raia masikini Burundi watasaidiwa na UM kupata vitambulisho vya kura bila malipo

Raia wa Burundi milioni moja, waliotimia umri wa kupiga kura, watafadhiliwa bure vitambulisho vya uraia vitakavyowaruhusu kushiriki kwenye uchaguzi utakaofanyika nchini mwao mnamo mwezi Mei 2010.

EU imechangisha Yuro milioni 5.5 kuisaidia UNRWA kuimarisha afya bora kwa wakazi wa Tarafa ya Ghaza

Ijumatatu, Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza kufadhilia msaada wa Yuro milioni 5.5 kulipa Shirika la UM Linalofarajia Misaada ya Kihali kwa WaFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA) uliokusudiwa kuhudumia miradi ya afya na mazingira safi kwenye Tarafa ya Ghaza.

Mkuu wa misaada ya dharura ahimiza hifadhi bora kwa raia wa JKK dhidi ya mashambulio ya waasi wa LRA

John Holmes, Naibu KM juu ya Masuala ya Kiutu na Mratibu wa Misaada ya Dharura, ametoa mwito maalumu unaopendekeza jamii ya kimataifa ichukue hatua za nguvu zaidi zitakazohakikisha raia wanaokabiliwa na hatari ya kushambuliwa na waasi wa Uganda, wa kundi la LRA, huwa wanapatiwa ulinzi na hifadhi inayofaa kuwanusuru kimaisha.

Matukio katika Baraza la Usalama

Baraza la Usalama asubuhi limepitisha azimio la kuiwekea vikwazo Eritrea. Azimio linapiga marufuku kuiuzia silaha Eritrea au kununua silaha kutoka taifa hili.

UNHCR yachapisha maelekezo kukabili utovu wa ustahamilivu na ubaguzi wa wageni wahamiaji

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limechapisha, kutoka Geneva, leo hii maelekezo maalumu ya kutumiwa kukabili matatizo ya ubaguzi wa rangi na chuki, dhidi ya wageni, matatizo ambayo husababisha watu kuhama na kuhatarisha juhudi za UNHCR katika kuwapatia hifadhi watu waliokosa uraia, wahamiaji na wale wenye kuomba hifadhi za kisiasa.

Mlinzi wa majengo ya UM Usomali auawa

UM imeripoti Ijumanne majambazi kadha walimpiga risasi na kumwua ofisa raia wa usalama nchini Usomali, aliyekuwa akitumikia Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP), kitendo kilichotukia kwenye mji wa Beledweyn, Usomali.

UNHCR imetangaza watu 74,000 wa Pembe ya Afrika wamehajiri Yemen 2009 kuomba hifadhi

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti raia 74,000 waliwasili kwenye mwambao wa taifa la Yemen mwaka huu, kutoka eneo la Pembe ya Afrika, watu waliokuwa wakikimbia hali ya mtafaruku uliozuka na kujiepusha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, pamoja na uegugeu wa kisiasa, hali duni ya maisha, ikichanganyika vile vile na baa la njaa na ukame.

Ripoti ya FAO yanonyesha bei za chakula zimeanza kupanda tena kwenye soko la kimataifa

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kwenye ripoti iliochapishwa Ijumatano kwamba bei za juu za chakula, zimeanza kupanda tena katika dunia.

WFP kutumia msaada Umoja wa Ulaya kufyeka utapiamlo mkali unaofukuta Kenya Kaskazini

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kwamba yuro milioni 7.5 (sawa na dola milioni 11.3) ilizopokea kutoka Idara ya Misaada ya Kiutu ya Kamisheni ya Mataifa ya Ulaya, zitatumiwa kuhudumia kihali matatizo ya utapiamlo wa kima cha juu, yaliojiri miongoni mwa watoto wadogo, mama wajawazito na mama wanaonyonyesha wanaoishi katika maeneo ya ukame, Kenya Kaskazini.