Msaada wa Kibinadamu

WFP itafadhilia posho ya mwezi kwa waathiriwa wa vurugu Goma

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza kwamba kuanzia Ijumatano ya kesho litaendeleza ugawaji wa posho ya chakula cha siku 10 kwa waathiriwa 135,000 ziada waliopo kwenye kambi sita za wahamiaji wa ndani karibu na mji wa Goma.

WHO imefadhiliwa na Norway tani 30 za madawa kuhudumia afya katika JKK

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kufadhiliwa na Serikali ya Norway msaada wa tani 30 za madawa, wa kuhudumia, kwa mwezi mmoja, watu 150,000 na kuwapatia matibabu dhidi ya maradhi ya kuharisha, butaa ya kihoro na kiwewe yanaozushwa na mapigano pamoja na maradhi mengineyo hatari, husuasan yale yanayotokana na maji machafu.~