Msaada wa Kibinadamu

Masuala kuhusu silaha ndogo ndogo, Sudan na Sahara ya Magharibi yajadiliwa na BU

Wajumbe wa Baraza la Usalama leo asubuhi walishauriana juu ya udhibiti bora, wa kimataifa, wa biashara ya silaha ndogo ndogo. Kadhalika Baraza lilizingatia masuala yanayohusu hali Sudan, na maendeleo katika shughuli za kuandaa kura ya maoni katika Sahara ya Magharibi.

WFP inaomba isaidiwe dola milioni 256 ziada kuhudumia chakula walimwengu

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza mwito maalumu wenye kupendekeza kufadhiliwa na wahisani wa kimataifa dola milioni 265 ziada, ili kukidhi mahitaji ya ule umma muhitaji wenye kuhudumiwa chakula na UM, katika sehemu kadha wa kadha za kimataifa. WFP ilisema msaada huu ziada unahitajika kununua chakula kwenye soko la kimataifa kufuatilia mfumko wa kasi wa bei za chakula uliojiri karibuni.~~

Akiba ya chakula Kenya kuharibiwa na kivu, OCHA yaonya

Ofisi ya UM juu Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba Kenya inakabiliwa kwa sasa na matatizo ya chakula kwa sababu ya kuharibika kwa mavuno ya mpunga yalioambukizwa na wadudu wa kuvu. Elizabeth Brys, Msemaji wa OCHA katika Ofisi ya UM Geneva aliwabainishia waandishi habari Ijumaa asubuhi juu ya tatizo hili:~

Moto umeharibu kambi za wahamiaji wa Darfur katika Chad mashariki

Kambi ya Goz Amer iliopo Chad mashariki, kilomita 70 kutoka Darfur, Sudan, Ijumaa ilivamiwa na moto ulioteketekeza vibanda viliotengenezewa vijiti na matope, makazi ya muda kwa wahamiaji wa Darfur 3,000.

Dereva na msaidizi walioajiriwa na WFP wauawa Sudan Kusini

Dereva aliyeajiriwa na Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) pamoja na msaidizi wake waliuawa Ijumatatu Sudan Kusini walipokuwa wanahudumia chakula umma muhitaji wa eneo hilo.

Waburundi 300,000 wamesaidiwa kurejea mwakao na UNHCR

Operesheni za Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) za kuwarejesha makwao, kwa khiyari, wahamiaji wa Burundi waliokuwa wakiishi kwenye kambi za muda ziliopo taifa jirani la Tanzania, kadhia zilizoanzishwa mwaka 2002, zilikamilisha kurejesha jumla ya wahamiaji 300,000 mnamo mwezi Machi mwaka huu.