Msaada wa Kibinadamu

UM unaomba msaada wa kuhudumia kihali waathiriwa 75,000 wa mafuriko Ghana

UM na washirika wake kadha wametoa mwito maalumu kwa jamii ya kimataifa unaopendekeza wafadhiliwe haraka dola milioni 10 ili kuhudumia afya, makazi na vifaa vya nyumba kwa watu 75,000 walioathirika na mafuriko Ghana kaskazini. Mafuriko haya yalioselelea tangu Agosti yalisababishwa na maji kujaa kwenye Mito ya Volta Nyeupe na Nyeusi.

Liberia inastahili msaada wa Mfuko wa Ujenzi wa Amani: asema KM

KM Ban Ki-moon amepitisha mwito unaothibitisha kwamba Liberia inastahili kupokea msaada wa fedha za maendeleo kutoka Mfuko wa UM juu ya Ujenzi wa Amani. Kadhalika KM ameliamrisha Shirika la Ulinzi wa Amani la UM katika Liberia (UNMIL) lianze kushauriana na wenye madaraka Liberia pamoja na mashirika ya kiraia na kuandaa ni miradi gani itafaa kupewa umbele katika kupokea misaada hiyo ya UM.

WFP kununua mahindi Lesotho kusaidia Liberia

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kununua mahindi kutoka wakulima wadogo wadogo wa Lesotho, mahindi ambayo yatatumiwa kuwapatia chakula na lishe bora kwa maelfu ya watoto wa skuli za praimari katika Liberia.

UM inahitajia kufadhiliwa msaada ziada wa kijeshi kwa Darfur

Idara ya UM juu ya Operesheni za Ulinzi wa Amani Duniani (DPKO) imeripoti kutofanikiwa kufadhiliwa na nchi wanachama misaada ya vifaa na zana nzito nzito za kijeshi, pamoja na helikopta, vifaa ambavyo vinahitajika kutumiwa na vikosi mseto vya Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa, vitakavyojulikana kama vikosi vya UNAMID, vitakavyopelekwa Darfur, Sudan mwisho wa mwaka.

Katibu Mkuu ameitisha mkutano wa aina ya pekee kuimarisha maendeleo Afrika

Ripoti ya mwezi Juni (2007) ya Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) ilibainisha mataifa ya Afrika yaliopo kusini ya Sahara bado yamepwelewa sana kwenye juhudi za maendeleo, kwa ujumla, na hakuna dalili haya yatafanikiwa kuyakamilisha, kwa wakati, yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) ya kupunguza kwa nusu, kabla ya 2015, umasikini, njaa, maradhi na kutojua kusoma na kuandika.

Mkuu wa UM juu ya misaada ya dharura kutilia mkazo umuhimu wa suluhu ya kisiasa DRC

Mnamo mwanzo wa wiki, John Holmes, Naibu KM juu ya Misaada ya Dharura aliripoti kwenye kikao cha faragha cha Baraza la Usalama juu ya hali ya kiutu kijumla katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) baada ya kulizuru eneo hili la Afrika ya Kati.

Masaibu ya wahamaji wa Pembe ya Afrika yaomba suluhu ya kimataifa

Shirika la Kimataifa juu ya Wahamaji (IOM) limeripoti kuwa linahitajia kufadhiliwa msaada wa dharura najamii ya kimataifa, utakaoliwezesha kununua vifaa vya kusajili na kuhifadhi takwimu za wale wahamaji na watu wenye kuomba hifadhi ya kisiasa kutoka eneo la Pembe ya Afrika, ambao wameanza kuwasili kwa wingi katika Yemen hivi karibuni baada ya kuvuka Ghuba ya Aden.

WFP inaomba dola milioni 80 kusaidia chakula wahamiaji Chad

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa mwito wa dharura, wiki hii, wenye kuitaka jumuiya ya kimataifa kuchangisha dola milioni 80 kusaidia chakula wahamiaji na wahajiri wa ndani ya nchi 400,000 waliopo Chad mashariki. WFP ilisema mchango huu unahitajika mwezi ujao, ili kuhakikisha kutakuwepo chakula cha kutosha kwa umma muhitaji kabla ya majira ya mvua kuwasili.

Upungufu wa fedha unahatarisha aila za Sahara Magharibi mipakani Algeria

UM imetangaza kuwepo upungufu wa asilimia 50 wa msaada wa fedha zinazohitajiwa kuhudumia aila za raia wa Sahara ya Magharibi, waliotengwa na jamii zao na ambao sasa huishi katika kambi za wahamiaji ziliopo Tindouf, Algeria.

Mtaalamu wa UM juu ya Haki za Watoto anazuru Cote d'Ivoire

Radhika Coomaraswamy, Mjumbe Maalumu wa UM anayehusika na Haki za Watoto kwenye Mazingira ya Vita, wiki hii ameanza ziara rasmi katika Cote d’Ivore, baada ya kuitika mwaliko wa Serekali ya taifa hilo. Coomaraswamy alitarajiwa kuendeleza ukaguzi juu ya utekelezaji wa miradi ya kuwarudisha, kwa jamii zao, wale watoto walioshiriki kwenye mapigano. Kadhalika Coomaraswamy anatazamiwa kusailia vitendo karaha cha kutumia mabavu kuwaingilia baada ya vita kumalizika.