Msaada wa Kibinadamu

Makundi ya wanamgambo 3,500 katika Ituri kukubali kusalimisha silaha

Makundi matatu ya wanamgambo wa JKK katika wilaya ya Ituri, yaani Mouvement Revolutionnaire Congolais (MRC), Front de Résistance Patriotique de l’Ituri (FRPI) na Front des Nationalistes et Intégraionnistes (FNI) yameahidi kusajili jumla ya wapiganaji wao 3,500 kwenye ule mpango wa UNDP ujulikanao kama mradi wa DDR, mpango ambao utawawezesha wanamgambo husika kupatiwa msaada wa fedha za kuanzisha maisha mapya ya kiraia au kujiunga na jeshi la taifa.

Juhudi za kuisaidia Uganda kukabiliana na mafuriko.

Ofisi ya UM inayohusika na Misaada ya Dharura, au Ofisi ya OCHA, imeripoti kwamba eneo la Uganda mashariki limekabwa na mafuriko makubwa baada ya mvua kali kunyesha katika mwisho wa Julai.

Waathiriwa wa mafuriko milioni 1.5 katika Sudan kufadhiliwa dola milioni 8.7 na UM

Waathiriwa milioni 1.5 (moja na nusu) wa mafuriko yaliotukia karibuni Sudan watafadhiliwa msaada wa dola milioni 8.7 kutoka ule Mfuko Maalumu wa Misaada ya Dharura wa UM, yaani Mfuko wa CERF. Fedha hizi zitatumiwa kupeleka misaada ya kiutu na kukidhia mahitaji ya dharura ya umma husika nchini Sudan.

UNHCR yajaribu kutafuta suluhu ya muda mrefu kwa raia wa Eritrea

Shirika la UM juu ya Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kuwa hivi sasa linashiriki kwenye jitihadi za kimataifa za kutafuta suluhu ya muda mrefu kwa raia wa Eritrea 130,000 waliokwama katika kambi 12 za wahamiaji ziliopo Sudan mashariki.

Miradi inayosaidiwa na UNICEF yawapatia Wa Misri maji masafi

Shirika la watoto la UM, UNICEF, na taasisi ya Coca Cola barani Afrika, wameungana kuimarishwa uwezeo wa huduma za maji kwa wa Misri wa maeneo ya mashambani na mijini.

Ajali ya treni huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Tukiendelea na makala ya Jarida wiki hii, kama mlivyo sikia kwenye taarifa ya habari kulitokea ajali mbaya ya treni huko karibu na mji wa Kakenge, jimbo la Kasai ya Magharibi DRC.