Msaada wa Kibinadamu

Juhudi za kuimarisha uzazi salama huko Tanzania

White ribbon alliance ni mungano wa kimataifa wa watu na mashirika uloundwa kuhamasisha wananchi juu ya haja ya kuwepo na afya nzuri na usalama kwa wanawake wote wajazito na wanapojifungua pamoja na watoto wanaozaliwa.

Mzozo wa Darfur unavyosababisha matatizo ya usalama kwa majirani wa Sudan.

Wakati majadiliano yanaendelea kwenye baraza la usalama katika kumaliza kuandika azimio litakalo ruhusu kupelekwa kwa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Jumuia ya afrika huko Darfur, mzozo huo katika eneo la magharibi ya Sudan umekua na athari kubwa kwa majirani zake Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Msaada wa kwanza wa Zambia kwa WFP unasaidia kupunguza upungufu wa chakula.

Program ya Chakula Duniani WFP, imepongeza mchango wa kwanza kabisa kutoka kwa serekali ya Zambia, ambao utawawezesha maelfu ya wa Zambia kupokea msaada muhimu wa chakula baada ya Septemba.

UM kusaidia polisi wa Liberia kufikia viwango vya kimataifa vya haki za binadam.

Mjumbe maalum wa UM huko Liberia amekabidhi kwa Kikosi cha Polisi cha Taifa, jengo lililo karabatiwa upya la kuwaweka wafungu kulingana na masharti muhimu kabisa ya viwango vya kimataifa vya haki za binadam.

Mkuu wa huduma za dharura wa UM yuamulika atahri za ukame huko Kusini mwa Afrika.

Mratibu wa huduma za dharura wa UM, Bw John Holmes alimulika wiki hii atahri za ukame sugu unaokumba nchi kadhaa za Kusini mwa Afrika, akisisitiza kwamba hali ni mbaya zaidi huko Swaziland. Alisema wanatarajia matatizo makubwa ya ukosefu wa akiba ya chakula katika eneo hilo.

Kwa habari za hapa na pale

Mashirika ya huduma za dharura ya UM yanapeleka kwa haraka misaada ya chakula na afya kusini mwa Sudan ambako mvua kali mnamo siku za hivi karibuni zimesababisha mafuriko yaliyowathiri karibu watu elfu 10. Shirika la watoto la UM, UNICEF limeshapeleka mikoba midogo 1 500 madawa na vitu vya dharura, pamoja na chakula cha siku 15.

WFP yawasaidia wa Sudan baada ya mafuriko

Mpango wa Chakula Duniani WFP umeanza kazi za kutowa huduma za dharura kwa kupeleka chakula na misaada kwa watu walio ondolewa kutoka makazi yao kati kati ya Sudan kutokana na mafuriko ya hivi karibuni.

Wataalamu watoa mwito kutanzuliwa shida za kufikisha msaada Somalia

Waatalamu wawili huru wa UM wametoa mwito wa kuchukuliwa hatua za kimataifa kukabiliana na tatizo la ukosefu wa usalama, kukimbia kwa raia kutoka makazi yao na uharamia, mambo yanayo zuia juhudi za kuwapelekea msaada wa chakula kwa maelfu ya wa Somali wanaokabiliwa na utapia mloo.