Msaada wa Kibinadamu

Sudan kupatiwa msaada wa ngano wa dola miloni mbili kutoka Urusi: imeripoti WFP

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP), limepokea kutoka Urusi, msaada wa ngano, wa dola milioni 2, uliokusudiwa kufufua tena zile operesheni za kuwapatia chakula watoto wa skuli muhitaji karibu 300,000 waliopo kwenye majimbo matatu ya Sudan yaliokabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula.

WFP imeanzisha operesheni za kuhudumia waathiriwa wa kimbunga Bukini

Shirika la WFP limeanzisha misafara ya ndege, za kupeleka chakula na misaada ya dharura inayohitajika kuwahudumia kihali maelfu ya watu wanaoishi kaskazini-magharibi ya Bukini, eneo ambalo hivi karibuni lilichafuliwa vibaya na kimbunga kilichoharibu vibaya sana barabara na madaraja.

KM kulitaka Baraza la Usalama (BU) kuanzisha mazungumzo ya amani kwa Sahara ya Magharibi

Ripoti ya karibuni ya KM juu ya Sahara ya Magharibi imependekeza kwa Baraza la Usalama kuwaita Morocco na Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi cha Frente Polisario, kushiriki, bila ya shuruti, kwenye mazungumzo ya kuleta suluhu ya kuridhisha, na ya kudumu, itakayoupatia umma wa Sahara ya Magharibi fursa ya kujichagulia serekali halali ya kuwawakilisha kitaifa.

Matatizo ya kiutu kukithiri katika CAR

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kwamba hali mbaya ya kiutu inaendelea kusambaa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) ambapo mamia elfu ya raia waliong’olewa makwao, kwa sababu ya hali ya vita na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, wanahitajia kufadhiliwa kidharura misaada ya chakula kunusuru maisha. Hali hii sasa hivi imechafuliwa zaidi kutokana na vurugu liliofumka na kufurika kutokea eneo jirani la Darfur, Sudan.

Mapigano makali Usomali kuzusha msiba mkuu wa kiutu nchini: OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba hali ya kijamii, kwa ujumla, katika Usomali, ni mbaya sana kwa sasa, kutokana na mapigano makali yalioshtadi karibuni, vurugu ambalo aina yake haijawahi kushuhudiwa tangu 1991.

Tume ya wataalamu wa UM kwenda Bukini kuratibu mradi wa kuwasaidia waathiriwa wa vimbunga

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imetuma Bukini timu maalumu ya wataalamu watano watakaofanya uchunguzi wa mahitaji ya kihali katika eneo hilo, na pia kuandaa utaratibu wa kuhudumia misaada ya kimataifa kwa umma ulioathirika na maafa ya vimbunga, maafa asilia ambayo yalileta uharibifu mkubwa kwenye taifa hilo la kisiwa.