Nchini Madagascar, mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kimataifa bado yanahaha kuwasaidia wananchi wa taifa hilo ambao kwa mfululizo katika kipindi cha muda mfupi mwezi uliopita wamepigwa na vimbunga vinne yaani Ana, Batsirai, Emnati na Dumako ambavyo vimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na ustawi wa watu. Ripoti iliyotolewa na serikali ya Madagascar inaonesha kwamba watu 400 000 wameathirika na vimbunga Emnati na Batsirai.