Msaada wa Kibinadamu

Msaada wa haraka unahitaji kwa wananchi waliozungukwa na maji ya mafuriko Sudan Kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeonya hali Sudan Kusini huenda ikawa mbaya zaidi ifikapo mwezi Mei mwaka huu iwapo msaada wa haraka hautapatikana kusaidia wananchi wanaoishi katika maeneo yakiyozingirwa na maji ya mafuriko ya muda mrefu.

Katika umri wangu wa miaka 70 sijashuhudia ukame wa kiwango hiki- Mwananchi Somalia

Akiwa amesimama mbele ya kibanda chake kwenye makazi ya wakimbizi ya Kulmiye wilayani Luuq nchini Somalia, Ahmad Hassan Yarrow anatazama kile kilichosalia katika mto Juba, ambao ulikuwa ndio tegemeo la uhai wa  eneo lao. Mto umekauka. “Katika umri wangu wa miaka 70 sijawahi kushuhudia ukame kama huu, katika vipindi vyote vya ukame vilivyopita,” anasema Bwana Yarrow katika makala iliyochapishwa kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini Somalia, UNSOM.

WHO yatoa huduma za matibabu na usaidizi wa kisaikolojia kwa wakimbizi wa Ukraine

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limejizatiti kuhakikisha wakimbizi kutoka Ukraine wanapatiwa msaada wa huduma za matibabu na usaidizi wa kisaikolojia.

UNHCR inahitaji dola bilioni 1.2 kwa ajili ya kutoa msaada kwa wakimbizi milioni 2.3 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumi wakimbizi, UNHCR limesema mzozo wa Sudan Kusini unasalia kuwa mzozo mkubwa zaidi wa wakimbizi huku asilimia 65 ya wakimbizi wakiwa ni watoto.

Baba akisalia Ukraine kupigana vita, mtoto ukimbizi na matumaini ya kumwona tena

Ni wiki mbili sasa tangu Urusi ianzishe mashambulizi yake nchini Ukraine, kitendo hicho kimesambaratisha familia ikiwemo wanaume kulazimika kusalia Ukraine ili kupigana vitani huku familia zao zikilazimika kukimbia maeneo mengine ya taifa hilo au hata nje ya Ukraine. 
 

Watoto wanauawa, wanajeruhiwa na wengine wanapata kiwewe kutokana na machafuko Ukraine: UNFPA

S​​​hirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA limesema kuongezeka kwa mgogoro nchini Ukraine kunaleta tishio la haraka na linaloongezeka kwa maisha na ustawi wa watoto milioni 7.5 wa nchi hiyo.

Shughuli za kusaidia wananchi walioathiriwa na vimbunga zinaendelea Madagascar

Nchini Madagascar, mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kimataifa bado yanahaha kuwasaidia wananchi wa taifa hilo ambao kwa mfululizo katika kipindi cha muda mfupi mwezi uliopita wamepigwa na vimbunga vinne yaani Ana, Batsirai, Emnati na Dumako ambavyo vimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na ustawi wa watu. Ripoti iliyotolewa na serikali ya Madagascar inaonesha kwamba watu 400 000 wameathirika na vimbunga Emnati na Batsirai.

Dola bilioni 1.7 zahitajika kukidhi mahitaji ya kibinadamu Ukraine:UN

Umoja wa mataifa na wadau wa masuala ya kibinadamu leo wamezindua ombi la dharura la jumla ya dola bilioni 1.7 ili kufikisha haraka msaada wa kibinadamu kwa watu nchini Ukraine na wakimbizi waliokimbilia nchi jirani