Msaada wa Kibinadamu

Tusisubiri baa la njaa litangazwe ndio tuisaidie Somalia: FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Somalia limetoa ombi la dola milioni 131.4 ili kusaidia wananchi 882,000 kutoka wilaya 55 wenye uhitaji wa haraka wa msaada wa kuokoa maisha yao. FAO wameisihi jumuiya ya kimataifa kutosubiri mpaka nchi hiyo itangaze kuwa na baa la ndio hatua zichukuliwe na badala yake wameomba hatua kuchukuliwa sasa.

Makubaliano yaliyotiwa saini leo Istanbul ni nguzo ya matumaini- Guterres

Hatimaye makubaliano ya kuruhusu meli zilizojaa shehena za nafaka kutoka nchini Ukraine zipite kwenye baharí nyeusi yamefikiwa hii leo huko Instanbul Uturuki baina ya Ukraine na Urusi yakishuhudiwa na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye amesema makubaliano hayo yameleta nuru kwa ulimwengu kupata ahueni kwenye bei za mazao ya chakula katika soko la kimataifa.

COVID-19 na Ukraine vimetulazimu tupunguze ukubwa wa chapati- Prince

Athari za kibiashara kutokana na COVID-19 pamoja na vita nchini Ukraine zinaendelea kusambaa duniani na zimebisha hodi hadi kwenye kambi ya wakimbizi ya Dzaleka nchini Malawi ambako ,mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amelazimika kupunguza ukubwa wa chapati ili angalau aweze kuendelea kutoa huduma hiyo pendwa kwa wakimbizi na wakati huo huo apate angalau faida kidodo ili akidhi mahitaji yake na aweze kujitegemea

Licha ya vikwazo, WFP yaendelea kuokoa maisha Haiti 

Nchini Haiti, ambako karibu nusu ya idadi ya watu tayari hawana uhakika wa chakula, njaa inatazamiwa kuongezeka huku kukiwa na ongezeko la mfumuko wa bei, gharama kubwa za chakula na mafuta na kuzorota kwa usalama, linaonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP ingawa linaendelea kutoa msaada kwa Wahaiti walio katika mazingira hatarishi.

Sasa hatuna wasiwasi tena mvua isiponyesha:Wakulima Mauritania

Mabadiliko ya tabianchi yanaleta madhara kila kona ya dunia ikiwemo kupungua kwa viwango vya mvua na hivyo kuleta usumbufu mkubwa wa wakulima, mathalan nchini Mauritani kiwango cha mvua kilichokuwa kikinyesha miaka 30 iliyopita sasa wanapata robo tu ya kiwango hicho hali iliyowatesa wakulima na wafugaji lakini mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo IFAD umewanusuru kwa kuwahakikishia maji mwaka mzima.

Mamia ya watu wapoteza maisha kwenye tetemeko la ardhi Afghanistan UN yajipanga kusaidia

Wadau wa kimataifa wa misaada ya kibinadmu yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa wanajiandaa kusaidia maelfu ya familia zilizoathirika zaidi na tetemeko kubwa la ardhi lililokubwa majimbo ya Paktika na Khost nchini Afghanistan mapema leo, mamia ya watu wameripotiwa kufariki dunia, wengi kujerihiwa wengine vibaya sana huku miundombinu ikiharibiwa vibaya.

Vita, Machafuko na majanga mengine vyatawanya watoto milioni 36.5 mwaka 2021: UNICEF 

Vita, machafuko na mjanga mengine vimewaacha watoto milioni 36.5 wakitawanywa kutoka majumbani kwao hadi kufikia mwisho wa mwaka 2021 kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambalo linasema idadi hiyo ni kubwa kabisa kurekodiwa tangu vita ya pili ya dunia.

Mtoto Charline atamani mapigano yaishe ili arudi Bunagana aendelee na masomo

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetembelea eneo la Rutshuru jimboni Kivu Kaskazini ili kutathmini hali ya mahitaji ya watoto na familia zao baada ya kufurushwa na kuhamia kwenye kambi za muda kufuatia mashambulizi kutoka vikundi vilivyojihami. 

Ukiona watoto wenye utapiamlo pembe ya Afrika utalia 

Mwaka 2011 dunia ilitangaziwa kuwepo kwa baa la njaa nchini Somalia ambapo zaidi ya watoto laki 340,000 walikuwa na utapiamlo, na ingawa mwaka huu bado baa la njaa halijatangazwa rasmi nchini humo lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema hali ni tete na watoto zaidi ya laki 380,000 wana utapiamlo mkali ambapo hata ukiwaona watoto hao machozi yatakutoka.

Mradi wa Sola wa UNICEF watatua changamoto za waathirika wa ukame Kori Ethiopia 

Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF wa kuweka paneli za sola kwa ufadhili wa mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umeleta nuru kwa maelfu ya waathirika wa ukame katika eneo la Kori jimboni Afar nchini Ethiopia hasa tatizo la maji.