Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) na lile la uhamiaji, IOM, wametoa wito wa pamoja kwa jamii ya kimataifa kutoa misaada zaidi ili kuitikia mahitaji ya wakimbizi na wahamiaji wa Venezuela katika nchi mbali mbali za ukanda wa Amerika Kusini.