Wahudumu wa mashirika ya misaada ya kibinadamu nchini Uganda wakiwemo wa Umoja wa Mataifa wanakumbana na changamoto kubwa ya kuwasaidia watoto wakimbizi zaidi ya 25,000 waliotengana na wazazi ama walezi wao kutokana na vita na kusaka hifadhi wakiwa peke yao nchini humo. Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego ametembelea makazi ya wakimbizi ya Imvepi Wialayani Arua nchini humo ambako kuna asilimia kubwa ya watoto na kuandaa tarifa hii.