Watoto wakimbizi nchini Rwanda sasa wanaona nuru katika maisha yao kutokana na ushirikiano kati ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na mfuko wa H&M.
Mkutano wa siku mbili wa kuchangisha fedha kusaidia Syria umeanza leo huko Brussels, Ubelgiji, wakati huu ambapo kuna ripoti ya kwamab maeneo yaliyokuwa yanazingirwa sasa yanafikika.
Kuwasikiliza na kuwashirikisha Wayemen katika mgogoro unaowahusu ni jambo la muhimu sana kwani suluhu ya vita nchini Yemen inaweza kutoka miongoni mwao na hasa kwa viongozi wao kuweka tofauti zao kando na kuafikiana sio kwa njia ya vita bali kupitia majadiliano.
Dhana potofu kuwa ulemavu ndio ukomo wa maisha imetupiliwa mbali huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Wakimbizi wa kike na wa kiume kutoka Burundi wamechukua hatua.
Teknolojia iwe ya hali ya chini au ya hali ya juu imekuwa mkombozi kwa mamilioni ya watu wenye uhitaji wa aina mbalimbali, kuanzia wakimbizi hadi wakulima limesema shirika la mpango wa chakula duniani WFP.
Ziara hii ya pamoja ni utekelezaji wa mpango wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Moussa Faki Mahamat wa kutaka pande mbili hizo zishirikiane katika kufanikisha ajenda zao za amani na maendeleo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM kwa ushirikiano na kampuni ya Panasonic Solar Lanterns, wametoa msaada wa umeme unaotumia nishati ya jua au wa sola kwa zaidi ya wakimbizi wa ndani 2400 nchini Ehtiopia.