“Hakuna suluhu ya kijeshi kwenye mzozo wa Syria,” amesisitiza tena hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres huku akitoa wito kwa kumalizwa kwa janga hilo lililosababishwa na binadamu na kuleta machungu ya muda mrefu kwa wananchi wa Syria.
Takribani watu milioni 6.5 nchini Sudan Kusini, ambao ni zaidi ya nusu ya watu wote wa Sudan Kusini, wanaweza kuwa hatarini kukumbwa na baa la njaa katika miezi ya Mei na Julai, yameonya mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa.
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo wamejulishwa kuwa mwaka huu wa 2020 utakuwa mwaka muhimu sana na wa kihistoria kwa wananchi na taifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.
Taarifa iliyotolewa hii leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura OCHA, imenukuu ripoti za kuaminika zisemazo kuwa mnamo tarehe 14 mwezi huu wa Februari, watu wenye kujihami kwa silaha waliwaua raia 20 wakiwemo watoto katika Kijiji cha Ntumbo, eneo la Kaskazini Magharibi mwa Cameroon.
Itakuwa gharama ndogo kwa sasa kulisaidia shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO kupambana na nzige Afrika Mashariki kuliko kuwasaidia mamilioni ya watu katika ukanda huo baada ya mazao yao yote kusambaratishwa, ameonya mkurugenzi mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP David Beasley.
Mvua kubwa zilizonyesha kwa wiki mbili zilizopita nchini Madagascar zimeathiri watu 120,000 ikiwakata kabisa na huduma za barabara, kusambaratisha shule 174, na kuwalazimisha watu 16,000 kusalia bila makazi.
Janga la nzige limeendelea kuliathiri eneo la Pembe ya Afrika hasa Ethiopia, Kenya na Somalia, lakini sasa wameripotiwa pia kubisha hodi Uganda na huku nchi za Sudan Kusini na Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizo katika tahadhari, kwa mujibu wa mratibu wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA.
Mashambulizi ya angani na ardhini ya jimbo la Idlib Kaskazini Magharibi mwa Syria yanasababisha wimbi kubwa la watu kutawanywa na Maisha ya raia kupotea na haya ni madhila ambayo hayastahili na yanapswa kukomeshwa sasa amesema Geir Pedersen mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria akitoa taarifa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo.