Msaada wa Kibinadamu

Watu 11,000 walazimika kusaka usalama Uganda wakikimbia mapigano DRC:UNHCR

Wimbi la mapigano mapya yaliyozuka Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC limewalazimisha takriban watu 11,000 kukimbia na kuvuka mpaka kuingia nchi Jirani ya Uganda kusaka usalama tangu Jumapili usiku limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. 

WFP yaonya watu milioni 3 zaidi sasa 'wanakabiliwa na makali ya njaa'

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limeonya kwamba idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa katika nchi 43, imeongezeka hadi kufikia milioni 45, yaani juu kwa ongezeko la watu milioni tatu mwaka huu huku njaa kali ikiongezeka kote ulimwenguni. 

Lazima kuwe na uwajibikaji katika ukiukwaji mkubwa wa haki Tigray:OHCHR Ripoti

Utafiti wa Pamoja uliofanywa na tume ya haki za binadamu nchini Ethiopia (EHRC) na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) umebaini kwamba kuna sababu za msingi za kuamini kwamba pande zote katika mzozo wa Tigray nchini Ethiopia kwa kiasi fulani wamekiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu, sheria za ubinadamu na sheria za wakimbizi, ukiukwaji ambao unaweza kuwa ni uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Baa la njaa labisha hodi Madagascar huku hatari kwa watoto ikiongezeka:WFP

"Madagascar hivi sasa iko katika hatihati ya baa la njaa kwa mujibu wa tathmini ya vipimo vya hali cha chakula imefikia daraja la tano (IPC 5) katika baadhi ya maeneo au hali kama njaa, na hii kimsingi ndiyo hali pekee labda  na ya kwanza ya njaa iliyochochewa na mabadiliko ya tabianchi duniani," amesema Arduino Mangoni, naibu mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP nchini Madagascar, akitumia tathmini za ukosefu wa chakula za IPC, ambazo ndio hutumika kupima kiwango cha usaidizi wa dharura unaohitajika.

Vita Sudan Kusini havijakatili maisha na kutawanya watu tu, pia vimewatowesha wengi:UNMISS

Vita vilivyodumu kwa zaidi ya miaka 10 sasa nchini Sudan Kusini vimeambatana na athari nyingi, mbali ya kukatili maisha ya maelfu ya watu, kuwatawanya mamilioni sasa watu wengi wanawasaka ndugu zao kwa udi na uvumba kwani hawajulikani waliko, wametekwa ama wametoweka kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS.

Tusaidie wanaopata madhara kutokana na dawa za kulevya: UNAIDS

Katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Watumiaji wa dawa za Kulevya, shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI UNAIDS linataka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya uhalifu wa watu wanaotumia dawa za kulevya, kuwasaidia wanaopata madhara yatokanayo na Virusi vya Ukimwi VVU, homa ya ini na masuala mengine ya afya, kwa ajili ya kuheshimu haki za binadamu na pia wameomba ufadhili zaidi wa programu za kupunguza madhara zinazoongozwa na jamii.

Watu milioni 5 wameaga dunia kwa COVID-19 , usawa wa chanjo utawaenzi: Guterres

Wakati dunia Jumatatu ya leo Novemba Mosi ikitafakari machungu ya COVID-19 kwa kupoteza maisha ya watu milioni 5, Katibu Mkuu António Guterres ametoa wito kwa viongozi wa kimataifa kuunga mkono mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kufanya usawa wa chanjo kuwa hali halisi kwa kuharakisha na kuongeza juhudi na kuhakikisha umakini wa hali ya juu ili kuvishinda virusi hivi.

Mshikamano wa kimataifa wahitajika kufikia amani na usalama Afrika:UN

Naibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo amesisitiza umuhimu wa amani na usalama barani Afrika, wakati akiwashukuru mabalozi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kusaidia Umoja wa Mataifa kuangazia suala hilo, na jinsi nchi zote wanachama zinavyoweza kufanya kazi na Muungano wa Afrika AU, kanda zingine na vikundi vya kanda, ili kufanya maisha kuwa salama zaidi katika bara zima.

Tetemeko la ardhi la karibuni limewajengea mnepo Wahaiti

Raia wa Haiti ambao waliathiriwa na tetemeko kubwa la ardhi lililopiga kusini magharibi mwa nchi mwezi Agosti mwaka huu wameonesha "ustahimilivu na mnepo wa hali ya juu" kwa mujibu wa mfanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji (IOM), ambaye amekuwa mstari wa mbele na kuunga mkono juhudi za uokozi.

Zaidi ya wakimbizi 60,000 wa Burundi warejea nyumbani mwaka huu pekee

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema wakimbizi 343 wa Burundi waliokuwa wanaishi  nchini Uganda wamerejea nyumbani jana Jumatatu na hivyo kufanya idadi ya warundi waliorejea nyumbani mwaka huu pekee kuwa zaidi ya 60,000.