Msaada wa Kibinadamu

Nchi 15 za Afrika zafikisha lengo la kuchanja asilimia 10 ya watu wake dhidi ya COVID-19: WHO

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO leo limesema nchi 15 za Afrika ambazo ni karibu theluthi moja ya nchi zote 54 zimefanikiwa kuwachanja kikamilifu asilimia 10 ya watu wake dhidi ya COVID-19. 

Dunia ina wakimbizi wa ndani zaidi ya milioni 55: Ripoti yao yawasilishwa UN

Suluhu za kitaifa lazima zipatikane kwa watu zaidi ya milioni 55 waliotawanywa kwenye nchi zao kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na jopo la ngazi ya juu linalojikita na wakimbizi wa ndani. 

WHO na UNICEF wazindua kitabu cha watoto kuhusu COVID-19

Kitabu kipya kilichopewa jina “Shujaa Wangu ni Wewe 2021” au “My Hero is You 2021” ambacho kimezinduliwa mwishoni mwa wiki na mashirika ya kibinadamu yakiwemo ya Umoja wa Mataifa kina lengo la kuwapa Watoto matumaini ya kuendelea na maisha hasa wakati huu wa janga la corona au COVID-19 limesema shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na lile la kuhudumia Watoto la UNICEF. 

Wiki ya hali ya hewa Afrika inalenga kuchagiza kasi ya kikanda kuelekea: UNCAC

Wiki ya vikao vya hali ya hewa barani Afrika 2021 imeanza leo Jumatatu kwa wito wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka kwa sauti muhimu kwenye ukanda huo. 

Wanasiasa wasomi Sudan Kusini wapora mamilioni ya dola na kuchochea ukiukwaji wa haki na machafuko:UN

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wamesema hatua ya viongozi wasomi nchini Sudan Kusini ya kuhamisha kinyume cha sheria fedha nyingi na rasilimali zingine za umma wanadhoofisha haki za binadamu na kuhatarisha usalama.

Miongo miwili baada ya azimio la Durban vita dhidi ya ubaguzi wa rangi vinaendelea:UN

Miongo miwili baada ya kupitishwa azimio la Durban ambalo lengo lake kuu lilikuwa ni kutokomeza ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa aina zingine, jinamizi hilo bado linaighubika dunia na vita dhidi yake vinaendelea. 

Changamoto zetu haziwezi kutatuliwa kwa mtutu wa bunduki: Biden

Nguvu za kijeshi za Marekani zinapaswa kuwa ni suluhu la mwisho kutumikana sio suluhu ya kwanza, amesema Rais wa Marekani Joe Biden alipowahutubia  viongozi wa dunia katika mkutano mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA76 mjini New York Marekani. 

Unaelewa nini kuhusu fedha kwa kukabili mabadiliko ya tabianchi?

Je unaposikia nchi zilizoendelea zinahamasishwa kutoa fedha kufanikisha miradi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi unaelewa nini?. Je ni nani anasimamia fedha hizo, zinatumika kwenye maeneo gani? nani ananufaika na fedha hizo na uamuzi wa kuanza kuchanga ulitokea wapi?

Hatupaswi kukata tamaa, tuna nia ya kujinasua kutimiza SDGs:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameiasa dunia kutopoteza matumaini hata kama mambo yanakwenda kombo katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs ili kutimiza lengo ifikapo mwaka 2030. 

Fedha za IMF kuwezesha Tanzania kujenga viwanda vidogo 7 vya hewa tiba ya oksijeni

Tanzania imesema imejipanga kuanza ujenzi wa viwanda vidogo 7 vya kutengeneza hewa tiba ya oksijeni ili kupambana na janga la Corona