Msaada wa Kibinadamu

Msaada wa kwanza wa vifaa tiba wawasili Afghanistan:WHO 

Ndege iliyobeba dawa na vifaa vya vingine vya afya vya kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO imewasili Afghanistan leo, 30 Agosti, majira ya jioni kwa saa za nchi hiyo. 

Watoto Afghanistan wako hatarini zaidi sasa kuliko wakati mwingine wowote:UNICEF

Chondechonde hatuwezi kuwatelekeza sasa watoto wa Afghanista kwani mahitaji yameongezeka zaidi  kuliko hapo awali, amesihi afisa mwandamizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) leo baada ya kuhitimisha ziara yake nchini humo.

UNICEF yatangaza kupanua huduma kwa wanawake na waoto nchini Afghanistan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema linaongeza programu zake za kuokoa maisha ya watoto na wanawake nchini Afghanistan ikiwa ni pamoja na kupitia huduma za afya, lishe na maji kwa familia zilizoyakimbia makazi yao. 

IOM yaomba wadau kuchangia dola milioni 15 kuisaidia Haiti

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limezindua ombi maalum la kukusanya dola milioni 15 kwa ajili ya kusaidia uongozi wa nchi ya Haiti kwenye suala la makazi ya muda, msaada wa afya ya akili na kinga dhidi ya COVID-19 kwa familia zaidi ya 137,000 zilizoathiriwa na tetemeko la ardhi lililotokea kusini mwa nchi hiyo .

WHO na UNICEF zataka kuanzishwa kwa safari za ndege maalum kupeleka misaada Afghanistan

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametaka kuanzishwa mara moja kwa daraja maalum la safari za ndege la kuwezesha ndege zilizobeba misaada ya kibinadamu kuingia nchini Afghanistan kwa ajili ya utoaji wa msaada endelevu na bila vizuizi. 

Majanga yaliyowapata wananchi wa Haiti ni fursa ya kuanza upya: Amina Mohamed

Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed amefanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Haiti na kusema msaada wanaoupata nchi hiyo baada ya kukumbwa na majanga ya tetemeko la ardhi unatoa fursa kwao kuunda mshikamano mkubwa wa kitaifa na kupanga njia mpya ya kusonga mbele.

WHO yaonya kuhusu kukata huduma za matibabu kwa mamilioni ya watu nchini Afghanistan

Uwasilishaji wa misaada ya kuokoa maisha na vifaa vya matibabu kwa mamilioni ya Waafghanistan haupaswi kukatwa, limeonya leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, likitaja kuongezeka kwa zaidi ya mara tatu ya idadi ya visa vya watu wanaokumbwa na kiwewe.

Idadi ya waliopoteza maisha ikiongezeka Haiti misaada ya UN yaanza kuwasili

  • Waliopoteza maisha baada ya tetemeko wazidi 700
  • Kimbunga Grace kinatarajiwa kuipiga nchini hiyo leo usiku
  • UNICEF na IOM zaendelea kutoa misaada wa kibinadamu

Katibu Mkuu wa UN atoa wito kwa pande zote Afghanistan huku  Baraza la Usalama likitegemewa kukutana Jumatatu hii. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anafuatilia hali ilivyo huko Afghanistan akiwa na wasiwasi mkubwa na amewasihi Taliban na wahusika wote wajizuie kwa kiwango cha juu ili kuepusha madhara kwa raia na pia kuhakikisha utoaji wa misaada ya kibinadamu. 

Tunafuatilia kwa ukaribu sana hali ya watu wa Haiti kufuatia tetemeko la ardhi - UN 

Umoja wa Mataifa unafanya kazi kusaidia juhudi za uokoaji na misaada nchini Haiti kufuatia tetemeko kubwa ambalo limesababisha mamia ya vifo, kujeruhi na huku wengine wakiwa hawafahamiki waliko na limesababisha uharibifu mkubwa katika sehemu ya kusini-magharibi mwa nchi.