Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limesema linaendelea kutiwa hofu na taarifa za kulazimishwa kurejea nyumbani kwa familia kutoka Msumbiji zilizokimbilia Tanzania.
Idadi ya watu waliopatiwa msaada wa chakula na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP huko jimboni Tigray nchini Ethiopia tangu mwezi Machi mwaka huu imefikia milioni moja.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema msaada wa haraka wa kibinadamu unahitajika kuwasaidia maelfu ya watu walioathirika na mlipuko wa volcano iliyolipuka tarehe 22 Mei mwaka huu kwenye mlima Nyiragongo mjini Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.