Idadi ya Watoto chini ya miaka 5 wanaougua utapiamlo mkali nchini Haiti inaweza kuongezeka zaidi ya mara mbili mwaka huu, ameonya Jean Gough mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto – UNICEF katika ukanda wa Amerika kusini na karibiani, wakati akihitimisha ziara yake ya siku 7 katika nchi hiyo.
Shirika La Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani, UNFPA limeongeza idadi ya watendaji wake kwenye jimbo la Tigray nchini Ethiopia kwa lengo la kusaidia mamia ya maelfu ya wanawake na barubaru wa kike kupata huduma za dharura za afya na ulinzi.
Maelfu ya wakazi wa mji wa Goma ulioko jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hawana makazi hivi sasa na wako kwenye harakati za kuhama hata kule walikokimbilia karibu na mji huo bada ya mamlaka kuwaagiza wahame kwa hofu ya kwamba volkano katika Mlima Nyiragongo inaweza kulipulka tena.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM na wadau wake wa masuala ya kibinadamu wamesambaza misaada ya dharura kwa familia za watu ambao wamelazimika kukimbia makwao kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na kuongezeka kwa kina cha maji cha Ziwa Tanganyika na mto Rusizi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, limelaani vikali uporaji wa chakula chake cha msaada na uharibifu wa ghala lake la kuhifadhi misaada ya kibinadamu kwenye eneo la Pobor jimboni Jonglei nchini Sudan Kusini.
Mashirika ya kutoa misaada na wadau wa Umoja wa Mataifa, wamelaani vikali kile walichokiita ni mwenendo wa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wafanyakazi wa misaada, na mashambulizi kwenye matukio mawili yaliyofanywa tarehe 21 Mei mwaka huu nchini Sudan Kusini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza masikitiko yake kufuatia vifo, majeruhi na uharibifu wa mali uliosababishwa na mlipuko wa volkano katika mlima Nyiragongo, huko Goma jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP limeimarisha msaada wa chakula katika maeneo yanayokabiliwa na njaa nchini Yemen kama sehemu ya kuzuia baa la njaa lakini uwezo wa shirika hilo kuendelea na shughuli hadi mwishoni mwa mwaka ziko njia panda.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, leo Jumapili limesema kwamba mamia ya watoto na familia katika mjini Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC wako katika hatari kufuatia mlipuko wa volkano wa Mlima Nyiragongo.