Umoja wa Mataifa umeelezea masikitiko yake kufuatia matokeo ya ahadi zilizotolewa katika mkutano wa kimataifa wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia Yemen mwaka huu wa 2021 ambayo inakabiliwa na janga la kibinadamu, linalotajwa kuwa kubwa zaidi duniani. Makisio yalikuwa dola bilioni 3.85 lakini iliyopatikana ni takribani dola bilioni 1.7.