Hali mbaya ya kibinadamu na ambayo inazidi kudorora” inayoathiri wanawake na watoto kaskazini magharibi mwa Syria imekuwa suala kuu kwa Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock ambaye amezungumza na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa hii leo jumatano mjini New York, Marekani.