Mashirika manne ya misaada ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s yanayofanya kazi kusaidia ukanda wa Sahel leo yameonya kwamba watu milioni 24, nusu yao wakiwa ni watoto wanahitaji msaada wa kuokoa maisha na ulinzi.
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA ametoa wito wa kuchukuliwa hatua Madhubuti ili kuepuka athari kubwa za mlipuko wa janga la corona au COVID-19 wakati akitoa ombi la dola bilioni 6.7 huku akieleza mipango ya kimataifa ya kupambana na virusi vya corona katika nchi zisizojiweza.
Nchini Uganda, ambako kuna wagonjwa 56 wa COVID-19, Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Rosa Malango hii leo amezindua ombi la dharura la dola milioni 316 za Marekani kwa ajili ya kushughulikia janga hili.
Wakuu wa mashirika makubwa ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadammu na ofisi mbalimbali leo wamezindua ombo la dharura kwa ajili ya kukusanya dola milioni 350 kusaidia vituo vya kimataifa vya misaada kwa ajili ya watu walio katika hatari zaidi wakati huu wa janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.
Ndege ya kwanza ya mshikamano ya Umoja wa Mataifa inatarajiwa kuondoka leo mjini Addis Ababa Ethiopia kuelekea nchi mbalimbali za Afrika ikiwa imesheheni msaada na vifaa ya kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona au COVID-19.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo jumapili kupitia msemaji wake, ametuma salamu zake za rambirambi pamoja na kusikitishwa kwake kutokana na kimbunga Harold ambacho kimezipiga nchi za visiwa vya Pacific na kusababisha upotevu wa maisha na mali.
Zimbabwe ambayo tayari ina matatizo makubwa ya chakula kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na mdororo wa uchumi sasa janga la mlipuko wa virusi vya Corona unatishia kutumbukiza mamilioni ya watu wa nchi hiyo katika janga la njaa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP.
Umoja wa Mataifa na washirika wake wa masuala ya kibinafdamu nchini Somalia wanaweka mipango na vipaumbele vipya ili kusaidia taifa hilo la Pembe ya Afrika katika maandalizi na hatua za kupambana na virusi vya Corona COVID-19.
Kama ilivyo kwingine kote duniani, walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanakabiliana na changamoto zinazoletwa na mlipuko wa virusi vya corona, COVID-19. Lakini kazi yao inaendelea na wanaendelea kutekeleza majukumu yao muhimu ya amani na usalama.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA leo limesema hatua za kupambana na kusambaa kwa virusi vya Corona , COVID-19 zinaathiri fursa, ufikishaji wa misaada na huduma za kibinadamu nchini Sudan.