Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limesema vita vya silaha na athari za kiuchumi na kijamii zilizosababishwa na janga la corona au COVID-19 vimefanya hali ya Watoto kuwa mbaya zaidi katika ukanda wa Sahel.
Wafanyakazi wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM wamesaidia mamlaka za Djibouti katika kusaka na kuzika mabaki ya wahamiaji wanane waliozama mwishoni mwa wiki na kisha miili yao kusombwa hadi fukweni wakati wakitoka Yemen .
Sudan inakabiliwa na zahma mbili kubwa ya mafuriko na mfumuko wa bei kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA.
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP , limefikisha msaada wa chakula uhaohitajika haraka kwa maelfu ya watu walioathirika na mafuriko Jonglei Sudan Kusini ili kuwaepusha na janga la njaa.
Watu 650,000 wameathirika na mafuriko yanayoendelea nchini Sudan kufuatia mvua kubwa zilizoanza kunyesha tangu mwezi Julai na juma hili pekee watu wengine 110,000 wametawanywa na sasa wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu limesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada wa kibinadamu na masuala ya dharura OCHA.
Nchini Sudan mvua kubwa zimesababisha mafuriko na kuharibu miundombinu huku watu zaidi ya 557,000 wakiwa hawana makazi na nyumba zaidi ya 111,000 zikisombwa kwa maji.
Zaidi ya watu milioni moja wametawanywa na kuwa wakimbizi wa ndani na machafuko yaliyozuka upya nchini Burkina Faso, kwa mujibu wa ripoti ya mwezi Agosti ya baraza la taifa kwa ajili ya masuala ya dharura na misaada (CONASUR).
Wahudumu wa kibinadamu ni wanawake na wanaume mashujaa ambao hufikisha msaada wa kuokoa maisha kama malazi, huduma muhimu za afya, chakula, maji na huduma za usafi kwa watu wasiojiweza na walio hatarini, hivyo wanastahili kuheshimiwa na kupongezwa.
Umoja wa Mataifa leo umezindua ombi la dola milioni 565 ili kuwasaidia watu wa Lebanon kutoka katika msaada wa dharura wa kibinadamu wa kuokoa Maisha na kuingia katika hatua ya kujikwamua na ujenzi mpya na hatimaye kuelekea katika hatua za muda mrefu za kujikomboa kiuchumi kufuatia milipuko ya wiki iliyopita katika bandari ya Beirut.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kujikusanya na kugawa misaada ili kukidhi mahitaji ya waathirika wa mlipuko mjini Beirut. Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP hivi sasa linajiandaa kusafirisha maelfu ya tani za unga wa ngano ili kujaza ghala la chakula cha msaada lililosambaratishwa na mlipuko huo kwenye bandari ya Beirut.