Wanafamilia wa mwanamuziki nguli na wa kukumbukwa sana duniani, Bob Marley, wametangaza kuutengeneza upya wimbo maarufu wa Bob Marley unaofahamika kwa jina One Love ili waunge mkono kazi za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, kurejesha tena ulimwengu wa haki zaidi kwa watoto ambao maisha yao yamevurugwa na janga la COVID-19, imeeleza taarifa ya UNICEF iliyotolewa hii leo mjini New York Marekani.