Kufuatia tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.5 vipimo vya richer katika jimbo la Sulawesi Katikati mwa Indonesia siku ya Ijumaa , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshitushwa na janga hilo na idadi ya watu waliopoteza maisha na kujeruhiwa.
Sisi ni kizazi cha kutokomeza njaaTunaweza kuwa kizazi cha kwanza kufanikiwa kutokomeza njaa, kama ambavyo tunaweza kuwa kizazi cha mwisho kuikoa dunia.
Colombia inakabiliwa na zahma kubwa wakati huu ambapo maelfu ya raia wa Venezuela wanaendelea kumiminika nchini humo kutokana na ukosefu wa chakula na mahitani mengine ya msingi nchini mwao.
Kivuko chazama nchini Tanzania na kusababisha vifo, Umoja wa Mataifa umetuma salamu za rambirambi ukisema uko tayari kusaidia kwa kadri itakavyohitajika kufanya hivyo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza masikitiko yake makubwa kufuatia ripoti za vifo vya watu vilivyosababishwa na kimbunga Mangkhut nchini Ufilipino.
Mapigano katika mji wa bandari wa Hudaydah nchini Yemen ambayo yameharibu ghala la chakula la shirika la mpango wa chakula duniani, WFP yanatishia kudhoofisha jitihada za kulisha mamilioni ya watu katika nchi hiyo iliyoharibiwa na vita, amesema Herve Verhoosel msemaji wa WFP mjini Geneva Uswisi wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Colombia inaendelea kukabiliwa na janga wakati huu ambapo maelfu ya raia wa Venezuela wanaendelea kumiminika nchini humo kila siku kutokana na uhaba wa chakula, dawa na mahitaji mengine muhimu nchini mwao.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amelaani ongezeko la ghasia ndani na katika viunga vya mji mkuu wa Libya ,Tripoli, ambazo zimewaacha raia kadhaa wakipoteza maisha na wengine kujeruhiwa.