Msaada wa Kibinadamu

Halahala wanachama tushikamane kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina:UN

Tunasikitishwa na uamuzi wa  Marekani wa kusitisha ufadhili wa fedha kwa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Palestina UNRWA ambalo linawasaidia wakimbizi hao na kuchangia hali ya utulivu katika kanda hiyo, mesema Stephane Dijarric msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika taarifa iliyotolewa Ijumaa.

Ahueni kwa wahamiaji baada ya mkwamo Diciotti kumalizika

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeeleza furaha yake baada ya kumalizika kwa mkwamo wa wahamiaji 140 waliokuwa wamesalia kwa siku sita ndani ya meli ya uokozi ya Diciotti katika pwani ya Sicily nchini Italia.

Shambulio lingine lalenga watoto Yemen, OCHA yapaza sauti

Kwa mara nyingine tena ndani ya wiki mbili watoto nchini Yemen wameshambuliwa na kuuawa huko jimboni Hudaydah.

Wahusika wa mauaji ya raia huko Borno wasakwe na washtakiwe- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mauaji ya raia wakati wa ghasia zilizotokea huko jimbo la Borno, Kaskazini-mashariki mwa Nigeria.

Wahudumu wa kibinadamu waendelea kuuawa kila  uchao- Guterres

Hii leo ni siku ya kimataifa ya usaidizi wa kibinadamu ambapo Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa viongozi ulimwenguni kufanya kila wawezalo kulinda watu walionasa kwenye mizozo.

Ujasiri wa wafanyakazi wa UN wawezesha bendera yetu kupepea juu zaidi- Guterres

Bendera ya buluu ya Umoja wa  Mataifa inapepea juu kabisa kwa sababu ya ujasiri wa wanawake na wanaume ambao wanaipeperusha mbali zaidi hadi kona mbali zaidi duniani.

Heko watoa huduma kwa kuweka rehani maisha yenu kwa maslahi ya wengi- UNHCR

Hebu fikiria maisha ya walio kwenye mizozo kuanzia barani Afrika, Asia, Ulaya hadi Amerika yangalikuwa vipi bila watoa misaada ya kibinadamu wanaoweka rehani uhai wao?

UNRWA  yapata fedha lakini zatosha mwezi mmoja tu

Baada ya vuta nikuvute na kutokuwa na uhakika wa ufadhili kwa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada kwa wakimbizi wa kipalestina UNRWA, hatimaye kuna matumaini baada ya baadhi ya wahisani kujitokeza kusaidia angalau shule ziweze kufunguliwa mwezi ujao.

Watu 52,000 waathirika na ghasia jimboni Somali nchini Ethiopia :WFP

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa- WFP  limeanza  kusambaza chakula kwa mamia ya maelfu ya  watu wanaotafuta makazi ya muda baada ya kukimbia ghasia  katika jimbo la Somali nchini Ethiopia.

Ahsante EU kwa msaada wako kwa watu wa Gaza- WFP

Muungano wa Ulaya EU umelipatia shirika la mpango wa chakula duniani, WFP zaidi ya dola milioni 3 kwa ajili ya kusaidia kununua chakula cha wapalestina walioko ukanda wa Gaza  huko Mashariki ya Kati.