Msaada wa Kibinadamu

Hungary tupilieni mbali mswada wa sheria zitakayowaathiri wakimbizi: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limetoa wito kwa serikali ya Hungary kuachana na mswada wa sheria zinazotarajia kuwasilishwa bungeni ambazo zitabana uwezo wa mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s na watu binafsi kuwasaidia waomba hifadhi na wakimbizi.

IOM yasaidia kuwarejesha Ethiopia wahamiaji 100 Kutoka Yemen

Raia 101 wa Ethiopia waliokuwa wahamiaji nchini Yemen wameondoka kwa hiyari kwa msaada wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM na kurejea nyumbani kupitia bandari ya Hudaydah.

Watu milioni 1.9 CAR wahitaji msaada-OCHA

Jamhuri ya Afrika ya Kati-CAR,  inakabiliwa  na mgogoro mkubwa wa kibinadamu.  Mratibu wa masuala ya kibanadamu nchini humo amesema hali si shwari na usaidizi zaidi unahitajika ili kunasua wananchi walio taabani.

Hali ya kibinadamu si shwari Yemen : OCHA

Hali ya kibinadamu nchini Yemen inazidi kuzorota kutokana  kuongezeka kwa migogoro, vikwazo dhidi ya misaada ya kibinadamu na kupungua kwa uingizaji wa biashara muhimu hivyo kusababishwa mamilioni ya waYemen kukabiliwa  uhaba mkubwa wa chakula.

Juhudi dhidi ya Ebola DRC zijumuishe watoto- UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetaka harakati za kukabiliana na mlipuko wa Ebola huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ujumuishe watoto.

WHO na Benki ya Dunia waunda bodi kudhibiti milipuko ya magonjwa

 

Shirika la Afya ulimwenguni WHO na Benki ya dunia wameunganisha jitihada zao na kuunda bodi itakayosaidia kuimarisha usalama wa afya duniani.

Ulinzi wa raia vitani- maneno mengi kuliko vitendo

Mizozo kote duniani inaibua vitisho na machungu kwa mamilioni ya raia wakiwemo wanawake, wasichana, wanaume, wavulana na watoto.

Chanjo dhidi ya Ebola yaanza kutolewa Mbandaka

Chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola imeanza kutolewa hii leo kwenye jimbo la Equateur nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Poleni wafiwa katika ajali ya ndege Havana: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya ndege ya jana tarehe 18 mjini Havana  Cuba na kusababisha maafa kwa raia wengi.

UNICEF yachagiza mamia ya wahudumu kupambana na Ebola DRC

Katika hamasa ya kupambana na mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, leo shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, kwa ushirikiano na serikali na wadau, wanachagiza mamia ya wahudumu wa masuala ya kijamii kujiunga katika vita dhidi ya Ebola.