Ahadi ya dola zaidi ya bilioni 2 zimetolewa leo kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu nchini Yemen. Akitangaza jumla ya ahadi hizo kwenye mkutano wa kimataifa wa harambee ya Yemen mjini Geneva Uswis , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesisitiza kuwa rasilimali ni muhimu sana , lakini hazitoshi, cha msingi ni kuhakikisha zinawafikiwa watu wenye uhitaji, na ili hilo lifanikiwe inahitajika fursa ya kufika kila kona nchini Yemen bila vikwazo.