Msaada wa Kibinadamu

Ofisa mkaazi wa WHO anasema "hali ni ngumu tangu mashambulio kuanzishwa Ghaza"

Leo asubuhi tulipata taarifa ziada kutoka Mahmoud Daher, Ofisa wa Afya anayewakilisha Shirika la Afya Duniani (WHO) katika Ghaza, ambaye alihojiana, kwa kutumia njia ya simu, na Samir Imtair Aldarabi, mwanahabari wa Idhaa ya Kiarabu ya Redio ya UM. Daher alielezea hali ilivyo sasa hivi katika Ghaza, kama ifuatavyo:~

Mashirika ya UM yameanzisha kampeni ya kunusuru maisha kwa watoto wachanga na wanawake Usomali

Mashirika ya UM juu ya afya duniani, WHO, na huduma za maendeleo ya watoto, UNICEF, yameanzisha kampeni ya kuchangisha mamilioni ya dola zitakazotumiwa kwenye miradi ya kunusuru maisha ya watoto milioni 1.5, walio chini ya umri wa miaka mitano katika Usomali, pamoja na kuwasaidia wanawake wa umri wa kuweza kuzaa, yaani baina ya miaka 15 hadi 49, kujidhibiti kiafya.

Mifumko ya hali ya hewa mbaya ulimwenguni yakithirisha mahitaji ya wataalamu wa kudhibiti maafa

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba majanga yaliofungamana na athari za hali ya hewa mbaya duniani, katika mwaka 2008, ndio masuala na matatizo yaliotawala zaidi kwenye kazi na shughuli za kitengo cha UM juu ya Tathmini na Uratibu wa Maafa (UNDAC).

"Wahudumia misaada ya kiutu 100 ziada washambuliwa 2008 katika JKK": Holmes

John Holmes, Mshauri wa UM juu ya Masuala ya Kiutu na Misaada ya Dharura ameripoti kwamba katika mwaka 2008 wahudumia misaada ya kiutu katika JKK walishambuliwa zaidi ya mara 100, na baadhi yao hata waliuawa kutokana na hujuma hizo.

UNHCR yaomba milioni $92 kwa wahamiaji wa Usomali katika Kenya

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetoa mwito wa kutaka lifadhiliwe msaada wa dola milioni 92 ili kufarajia kihali Wasomali 250,000 waliosibika na matatizo ya makazi kwenye kambi kongwe za wahamiaji za Dadaab, ziliopo Kenya mashariki, karibu na mipaka na Usomali.

Tanzania kufunga kambi ya Nduta kwa wahamiaji wa Burundi: UNHCR

UNHCR pia imeripoti ya kwamba, kwa kulingana na mapendekezo ya UM, serikali ya Tanzania inajitayarisha mwisho wa mwezi kuifunga ile kambi ya Nduta, iliopo kaskazini-magharibi ya nchi, wanapoishi wahamiaji wa kutokea Burundi.

Waasi wa CNDP wakumbushwa na UNHCR kuhishimu haki halali za wahamaji waliopo Rutshuru katika JKK

Shirika la UNHCR limetoa mwito maalumu unaowataka waasi wafuasi wa kundi la CNDP la Laurent Nkunda, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) kuhakikisha raia waliomo kwenye maeneo wanayoyadhibiti wanapatiwa hifadhi na ulinzi, kwa kufuatana na kanuni za kiutu za kimataifa, hususan wale raia wahamiaji wa ndani ya nchi 10,000 waliopo karibu na kambi ya vikosi vya ulinzi amani vya UM vya MONUC, katika Rutshuru, [kilomita 80 kutoka mji wa Goma].

Hali inakhofiwa kuparaganyika Zimbabwe kwa kuwasili majira ya mvua, IFRC imehadharisha

Shirika la Kimataifa la Jumuiya za Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) limeripoti kukhofia hali Zimbabwe huenda ikachafuka zaidi kwa sababu ya majira ya mvua yanayonyemelea karibuni nchini.

EU yaanzisha ulinzi wa muda mrefu wa misaada ya kunusuru maisha Usomali

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa taarifa ya kuushukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa kupeleka manowari kwenye mwambao wa Usomali zitakazolinda zile meli zilizobebeba shehena ya misaada ya chakula dhidi ya maharamia.

UM wafanyisha kikao maalumu kuchangisha msaada ziada kwa Mfuko wa Maafa ya Dharura

Alkhamisi UM ulifanyisha kikao maalumu, cha mwaka, kuchangisha fedha zinazohitajika kufadhilia Mfuko wa UM juu ya Maafa ya Dharura au Mfuko wa CERF.