Haki za binadamu

KENYA: Heko Mahakama ya Afrika kwa uamuzi wa kulinda jamii ya Ogiek- Mtaalamu

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa jamii ya asili amepongeza uamuzi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu wa kuagiza serikali ya Kenya illipe fidia watu wa jamii ya asili ya Ogiek nchini humo kwa machungu na ubaguzi waliokumbana nao nchini humo.

UNMISS yapongeza hukumu kwa waliotenda utakili nchini Sudan Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS umekaribisha hatua zilizochukuliwa na serikali ya Sudan Kusini za kufuatilia na kutaka uwajibikaji kwa manusura wa ukatili wa kingono huko Yei, jimboni Equatoria ya kati. 

Wataalamu wa UN walaani ubaguzi dhidi ya wageni nchini Afrika kusini

Wataalamu wa ubaguzi na ubaguzi wa rangi wa Umoja wa Mataifa wamelaani kuongezeka kwa vitendo vya ubaguzi dhid ya raia wa kigeni nchini Afrika kusini na kutaka nchi hiyo ihakikishe kuna uwajibikaji dhidi ya ubaguzi kwa wageni, kauli za chuki na ubaguzi wa rangi.

UNMISS yaendesha mafunzo ya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS umeendesha mafunzo ya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji katika eneo la makutano la  Aru jimboni Equatoria ya Kati ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaandaa wananchi kujilinda kwa kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vimekuwa vikijirudia na kuathiri zaidi wanawake na wasichana. 

Mataifa ya Ulaya msiweke Watoto vizuizini:UN

Nchi za barani Ulaya zimeshauriwa kuacha kuwaweka Watoto wahamiaji vizuizini na badala yake watumie njia mbadala ambazo hazitasababisha Watoto hao kuathirika kisaikolojia, kuzidisha mfadhaiko na wasiwasi pamoja na unyanyasaji. Haya yamesemwa kwenye taarifa ya pamoja ya mashirika matatu ya umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la kuhudumia Watoto UNICEF na la uhamiaji IOM.

Ukatili wa kutisha waendelea kuripotiwa Tarhuna- Ripoti

Makaburi mapya yanayoshukiwa kuzika watu wengi kwa pamoja yamebainika huko Tarhuna nchini Libya, imesema ripoti mpya ya uchunguzi iliyotolewa leo na Tume Huru iliyoundwa na Baraza la  Umoja wa Mataifa la haki za binadamu.

Suriname inatoa “tumaini na msukumo kwa ulimwengu kuokoa misitu yetu ya mvua”: Mkuu wa UN

Suriname inaweza kuwa nchi ndogo na isiyo na watu wengi zaidi katika ukanda wa  Amerika ya Kusini, lakini ni moja ya nchi za kijani kibichi. Inachukuliwa kuwa kinara wa kimataifa katika uhifadhi wa bioanuwai, huku zaidi ya asilimia 90 ya ardhi yake ikifunikwa na misitu ya asili, rasilimali asilia isiyo na kifani ya taifa zaidi ya kufidia saizi yake.

Wahamiaji wafariki jangwani kwa kiu:IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesikitishwa na vifo vya wahamiaji wasiopungua 20 vilivyotokea katika jangwa la nchi ya Libya na kutoa wito  kwa mataifa ya Libya na Chad kuchukua hatua kali ili kulinda wahamiaji kwenye mpaka wa nchi hizo.

Jukumu la kusaidia wanawake wa Taliban ni letu sote: Bachelet

Umoja wa Mataifa umeusihi uongozi wa Taliban kukubali ombi la wanawake wanchi hiyo la kukaa nao na kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo haki zao za kibinadamu.

Ndoa za utotoni zashamiri Pembe ya Afrika - UNICEF

Watoto wa kike wenye umri mdogo hata miaka 12 huko Pembe ya Afrika wanalazimishwa kuolewa sambamba na kukeketwa au FGM, katika viwango vya kutisha wakati huu ambapo ukame mkali kuwahi kukumba eneo hilo katika kipindi cha miaka 40 ukisukuma familia katika mazingira magumu, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF.