Haki za binadamu

Arbour kukaribisha uamuzi wa Mahakama Kuu ya Marekani kuhusu wafungwa wa Guantanamo

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Louise Arbour ameripotiwa kukaribisha kwa ridhaa kuu uamuzi uliotolewa Alkhamisi na Mahakama Kuu ya Marekani kuhusu ile kesi ijulikanayo kama Kesi ya Boumediene dhidi ya Bush, uamuzi ambao uliidhinisha kwamba watuhumiwa wa kigeni waliowekwa kizuizini na Serikali ya Marekani, bila ya idhini ya mahakama, kwenye zile jela ziliopo katika Ghuba ya Guantanamo, Cuba kuwa nawo pia wana haki halali ya kufikishwa kwenye mahakama za kiraia kujitetea na mashitaka dhidi yao.

UM waadhimisha Siku ya Kupiga Vita Ajira ya Watoto Duniani

Tarehe 11 Juni huadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kupiga Vita Duniani Ajira ya Watoto wa Umri Mdogo. Taadhima za mwaka huu zimedhamiria kuamsha hisia za umma wa kimataifa juu ya umuhimu wa kuwapatia watoto wa umri mdogo elimu ya msingi.

ILO inapendekeza 'utandawazi unaohishimu haki za jamii'

Juan Somavia, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi wa Kimataifa (ILO) ametoa mwito uitakayo jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dharura katika kukabiliana na athari haribifu zinazoletwa na "msawazisho wa shughuli za uchumi katika soko la kimataifa uliokosa haki za kijamii". Alitoa pendekezo hilo wiki hii kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 97 wa ILO mjini Geneva.

Mtaalamu wa UM anakhofia athari za sheria mpya dhidi ya ugaidi Uingereza

Martin Scheinin, Mkariri Maalumu anayehusika na utekelezaji wa haki za binadamu kwenye mazingira ya ugaidi, ametoa taarifa maalumu, hii leo, yenye kuonya kwamba pindi Bunge la Uingereza litaamua mnamo Juni 11 kupitisha Mswada wa Kupiga Vita Ugaidi, anakhofia uamuzi huo utaathiri zile juhudi za kutekeleza haki za kimsingi, kimataifa, ikimaanisha nchi nyengine nazo pia zitataka kuigiza, na kuhalalisha sheria hiyo kwenye vyombo vyao vya sheria.

Wajumbe wa Baraza la Usalama wamewasili Cote d'Ivoire kukamilisha ziara ya Afrika

Tume ya wajumbe wa Baraza la Usalama wanaozuru Afrika imewasili Cote d\'Ivoire Ijumapili, wakiwa kwenye hatua ya mwisho ya ziara yao baada ya kutembelea mataifa ya Djibouti, Sudan, Chad na JKK. Ijumatatu wajumbe wa tume ya Baraza la Usalama wamefanyisha mazungumzo mjini Abidjan na Mjumbe Maalumu wa KM kwa Cote d\'Ivoire, Chuo Young-Jin na maofisa wengine wa ngazi za juu wa UM wanaohusika na huduma za amani nchini humo.

Wakati umewadia kukomesha kwa vitendo utumiaji mabavu dhidi ya Wanawake

Wiki hii Naibu KM Asha-Rose Migiro alipata fursa ya kuzungumzia suala la udhalilishaji wa kijinsia, kwenye mkutano maalumu uliotayarishwa mjini New York na Halmashauri ya Mataifa ya Ulaya pamoja na Ubalozi wa San Marino katika UM. Kwenye risala alioitoa mbele ya kikao hicho NKM Migiro alihimiza kuchukuliwe hatua za pamoja, kukomesha haraka tabia ya utumiaji nguvu na mabavu dhidi ya wanawake, hatua ambayo ikikamilishwa, alitilia mkazo, itawavua wanawake na mateso hayo maututi.~

Baraza la Haki za Binadamu linazingatia haki za wanawake

Louise Arbour, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu aliwaambia wajumbe waliohudhuria majadiliano ya Baraza la Haki za Binadamu (HRC) mjini Geneva, kuzingatia haki za wanawake kwamba bila ya kuwepo sheria za kuwakinga wanawake na mateso, pamoja na utumiaji mabavu dhidi yao, serikali za kimataifa na wote waliodhaminiwa madaraka ya utawala hawatofanikiwa kutekeleza usawa wa kijinsia kuimarisha maendeleo yao:~~

Louise Arbour ahutubia mara ya mwisho Baraza la Haki za Binadamu Geneva

Louise Arbour, Kamishna Mkuu wa UM Juu ya Haki za Binadamu Ijumatatu alihutubia mjini Geneva, kwa mara ya mwisho, Baraza la Haki za Binadamu kabla ya kustaafu. Alisema inatia moyo maenedeleo yaliopatikana kwenye juhudi za kuchunguza namna haki za binadamu zinavyotekelezwa miongoni mwa Mataifa Wanachama, hususan huduma za mapitio ya mara kwa mara.

Ofisa wa UM kuonya, vita, vurugu na uhasama huumiza mamilioni ya raia duniani

Naibu KM juu ya Masuala ya Kiutu, John Holmes aliwaambia wajumbe wa Baraza la Usalama Ijumanne kwamba fungu kubwa lenye kuathirika kihali na mali kunapojiri uhasama, vita na vurugu katika maeneo ya kimataifa ni mamilioni ya raia wasio hatia.

Naibu Kamishna Mkuu juu ya Haki za Binadamu azuru Cote d'Ivoire na Liberia

Naibu Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Kyung-wha Kang wiki hii ameanza ziara maalumu, ya pili, katika mataifa ya Cote d\'Ivoire na Liberia ambapo atafanya mazungumzo na viongozi wenye mamlaka, makundi yanayowakilisha jumuiya za kiraia, pamoja na wanadiplomasiya, na vile vile watumishi wa vyeo vya juu wa UM na kushauriana nao kuhusu hatua za kuchukuliwa kipamoja, zitakazohakikisha kadhia ya kuhifadhi haki za raia itatumiwa kuwa ni kipengele muhimu cha upatanishi miongoni mwa makundi yanayohasimiana, na pia katika kufufua kadhia za kiuchumi na jamii kwenye mataifa husika.