Leo ni maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kumbukizi na kutoa heshima kwa wahanga wa ugaidi duniani, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni fursa ya kusikiliza sauti zao pamoja na waathirika wa vitendo hivyo kama njia ya kufanikisha vita dhidi ya ugaidi duniani.