Haki za binadamu

Guterres amelaani machafuko yaliyosababisha vifo kwa waandamanaji Myanmar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo Jumapili amelaani vikali machafuko yaliyofanywa na vikosi vya usalama dhidi ya waandamanaji nchini Myanmar.

Haki ya kijamii inastahili pia katika uchumi wa kidijitali:UN 

Katika kuadhimisha siku ya haki ya kijamii duniani leo Februari 20, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa kuziba pengo la kidijitali lililozidishwa na janga la corona au COVID-19 na kuratibu kanuni za kazi katika majukwaa ya kidijitali. 

Tubadili mtazamo la sivyo safari ya kutokomeza ubaguzi wa rangi bado ndefu- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema safari ya kutokomeza ubaguzi wa rangi na madhila yatokanayo na kitendo hicho bado ni ndefu sana kwa kuzingatia kile kinachoshuhudia hivi sasa ulimwenguni kote.

Radio inakwenda na wakati kukidhi mahitaji ya jamii- UNESCO

Leo ni siku ya redio duniani, siku ambayo huadhimishwa kila tarehe 13 ya mwezi Februari kutoa fursa ya kuangazia mabadiliko, ubunifu na uunganishaji wa chombo hicho ambacho kimetimiza miaka 110.
 

Rudisheni mamlaka ya Myanmar kwa serikali iliyochaguliwa-Baraza la haki za binadamu. 

Kitendo cha jeshi kuchukua mamlaka kwa nguvu ni hatua kubwa kurudi nyuma kwa Myanmar, ambayo imekuwa katika njia ya kidemokrasia kwa miaka kumi iliyopita, amesema Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Nada An-Nashif wakati wa kikao cha Baraza na haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.  

Umoja, ubia na ushirikiano wa dhati ni muarobaini wa kutokomeza FGM

Umoja wa Mataifa umetaka ushirikiano katika ngazi zote na katika sekta zote za kijamii ili kulinda mamilioni ya wasichana na wanawake walio hatarini kukumbwa na ukeketeaji (FGM) kila mwaka.

Marekani kubadili mfumo wa kuomba hifadhi uhamiaji na kuunganisha familia. 

Shirika la Umoja la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limefarijika na hatua ya serikali ya Marekani, Jumannene kutia saini maagizo yanayolenga kutoa usalama na suluhu kwa wale wanaosaka hifadhi kwa misingi kwamba wanahitaji ulinzi kutokana na machafuko na mateso katika nchi zao. 

UN yasikitishwa na hukumu ya kifungo dhidi ya mpinzani wa kisiasa Urusi

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCR, imeelezea masikitiko  yake kufuatia hukumu ya kifungo dhidi ya mpinzani wa kisiasa na mwanaharakati nchini Urusi, Aleksei Navalny.
 

Tuna hofu na mwenendo wa kesi dhidi ya Dmitriev- Wataalamu UN

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa Urusi kuhakikisha kuwa kesi dhidi ya mtetezi wa masuala ya historia na haki za binadamu nchini humo Yuri Alexeevich Dmitriev inakuwa ya haki.

Waasi wa ADF na vikosi vya ulinzi vya DRC walishambulia raia 2020- Ripoti

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR, inasikitishwa na ongezeko kubwa la matukio ya mashambulizi ya raia kwenye maenoe ya Irumu na Mambasa jimboni Ituri halikadhalika eneo la Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.