Haki za binadamu

CERF yatoa dola milioni 15 ili kusaidia manusura wa tetemeko Indonesia

Umoja wa Mataifa umetoa dola milioni 15 kutoka mfuko wake wa msaada wa dharura kwa ajili ya kusaidia manusura wa tetemeko la ardhi na tsunami vilivyokumba eneo la Sulawesi nchini Indonesia tarehe 28 mwezi uliopita wa Septemba.

Tukiadhimisha siku ya kupinga machafuko, tufuate nyayo za Gandhi- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa dunia kufuata mtazamo na busara za Mahatma Gandhi katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga machafuko ambayo huangukia Oktoba Pili kila mwaka, siku ya kuzaliwa kiongozi huyo mashuhuri wa India aliyehamasisha vuguvugu la haki za kiraia kote duniani.

Tuimarishe ushirikiano wa kimataifa ili kunusuru uhamiaji- Grandi

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi ametoa wito kwa mataifa kushirikiana ili kupata ufumbuzi wa suala la wakimbizi akisema makubaliano mapya  kuhusu wakimbizi  yatageuza hifadhi kuwa jibu mujarabu.

Vijana mamlakani leo, ni wazee kesho! Pangeni mustakabali mnaotaka-Mtaalamu

Wakati kukishuhudiwa mabadiliko ya hali ya jamii, mchango wa wazee katika kuchagiza haki za binadamu ni muhimu sasa kuliko wakati mwingine.