Haki za binadamu

Siku ya kimataifa ya haki za binadamu, UM yawapongeza watu wanaosimama na kutetea haki

Huku siku ya kimataifa ya haki za binadamu ikisherekewa hii leo Umoja wa Mataifa imetumia siku hii kuwapongeza maelfu ya mashujaa ,na watetezi wa haki za binadamu ambao wanahatarisha maisha yao kuwatetea wengine.

Ban asisitiza umuhimu wa jamii ya kimataifa kuzuia kutokea kwa mauaji ya halaiki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki -moon amesisitiza kuwa kila nchi duniani inastahili kuchukua jukumu la kuzuia kutokea kwa mauaji ya halaiki.

UM wataka Liu Xiabao kuachiliwa huru

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya China kumuachiliwa huru mshindi wa tuzo la amani anayezuiliwa Liu Xiaobo.

UM watoa wito wa kuwepo kwa mbinu mpya kwenye mpango wa amani wa Mashariki ya Kati

Mratibu wa mpango wa amani katika eneo la Mashariki ya Kati amesema kuwa kuendelea na unjezi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi unaondeshwa na Israel katika ardhi wa Wapalestina kunahujumu mpango wa kutafuta amani katika eneo hilo.

Tamaduni zinazowadhulumu wanawake zatajwa kuwa nyingi nchini Afghanistan

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaotoa huduma nchini Afghanistan UNAMA unasema kuwa tamaduni zinazodhuru ambazo zinaenda kinyume na haki za wanawake na wasichana bado ni nyingi nchini Afghanistan zikiendeshwa kwenye jamii zote kote nchini.

Wanaopinga ubaguzi wasinyamazishwe:UM

Kundi la wataalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa watoa wito kwa mataifa kuchukua hatua dhidhi ya kuendelea kulengwa kwa wanaotetea haki za binadamu hali ambayo imesababisha vifo vya viongozi wa kijamii, mawakili , waandishi wa habari , wanaotetea wanawake na wengine wanaofanya jitihada za kumaliza ubaguzi na ukiukaji wa sheria.

Ni muhimu kuzidisha mapambano dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia wakati wa vita: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la visa vya ubakaji katika maeneo yanayokumbwa na migogoro, hivyo ametaka kuongezwa kwa nguvu ili kudhibiti vitendo hivyo na hata ikiwezekana kuwachukulia hatua kali wahusika wake.

Ban ataka kukomeshwa kwa vurugu nchini Haiti

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka kukomeshwa mara moja kwa vitendo vya vurugu nchini Haiti ambavyo vimezuka kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya awali ya ubunge.

Afisa wa UM ataka haki zaidi kwa wanawake

Kuanzishwa kwa kitengo maalumu ndani ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wanawake, kumeelezwa kuwa ni ukombozi tosha utakaoweza kuwakwamua wanawake hao.

Korea Kaskazi imeendesha vitendo vya uhalifu wa kivita:ICC

Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu kwenye mahaka inayohusika na uhalifu wa kivita ya ICC inasema kuwa imepokea habari kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini waliendesha vitendo vya uhalifu.