Haki za binadamu

Wakati kombe la dunia likifungua nanga leo IOM imezindua kampeni Msumbiji kuwalinda watoto

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM leo limekuwa msitari wa mbele katika kusaidia kampeni ya kitaifa nchini Msumbiji ya kutoa taarifa kuhusu usafirishaji haramu wa watoto.

UM waadhimisha Juni 12 ni siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto

Kila mwaka Juni 12 ni siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto na mwaka huu kauli mbiu ni "funga bao kutokomeza ajira ya watoto".

Ofisi ya UM ya haki za binadamu imesaini tena makubaliano na Nepal

Ofisi za haki za binadamu za Umoja wa Mataifa zimekubali ombi la serikali ya Nepal la kupunguza uwepo wake nchini humo kwa kufunga baadhi ya ofisi zake nje ya Kathmandu katika miezi ijayo.

ILO imetoa ripoti ya hali ya wafanyakazi eneo la Wapalestina linalokaliwa

Shirika la kazi duniani ILO linasema hali ya wafanyakazi katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa imeimarika kiuchumi.

Baraza la haki za binadamu limejadili masuala ya Iran mjini Geneva leo

Baraza la haki za binadamu linalokutana mjini Geneva leo linajadili tathimini ya matokeo ya Iran kuhusu utesaji.

Ban amesisitiza kutimiza malengo ya milenia barani Afrika

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye anaendelea na ziara barani Afrika amessisitiza umuhimu wa kutimiza malengo ya milenia.

UNICEF imeipongeza sekta ya utalii ya Afrikakwa kupambana na ngono kwa watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeipongeza sekta ya utalii ya Afrika ya Kusini kwa jitihada zake za kuhakikisha zinakomesha biashara ya ngono ya watoto katika sekta hiyo.

UNHCR imetoa wito wa kutowarejesha kwa nguvu wakimbizi wa Iraq

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa mataifa ya Uholanzi, Norway, Sweeden na Uingereza wanampango wa kuwarejesha nyumbani kwa nguvu wakimbizi wa Iraq baadaye wiki hii.

Mkuu wa haki za binadamu ataka mahakama maalum Kenya kuwahukumu wahusika wa ghasia za uchaguzi

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameitaka serikali ya Kenya kujaribu tena kuunda mahakama maalumu ili kukabiliana na wahusika wa ghasia za baada ya uchaguzi Desemba mwaka 2007.

Wapinzani nchini Burundi wapinga ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Wapinzani nchini Burundi wamekemea vikali ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon itakayoanza kesho Jumatano.