Haki za binadamu

Mjumbe Maalum wa KM kwa Usomali ana matumaini utulivu utarejeshwa nchini karibuni

Wiki iliopita Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji, Antonio Guterres, alibainisha kwamba tangu mapigano kufumka katika mji wa Mogadishu, mnamo mwanzo wa mwezi Mei, baina ya vikosi vya Serikali na makundi ya upinzani yaliojumuisha majeshi ya mgambo ya Al-Shabab na Hizb-al-Islam, watu 200,000 inaripotiwa walilazimika kuhajiri makazi, kiwango cha uhamaji ambacho kilishuhudiwa kieneo mara ya mwisho katika mwaka 2007, pale vikosi vya Ethiopia vilipoingilia kati, kwa nguvu, mgogoro wa Usomali.

UNICEF inajumuika na mashirika ya kiraia kuhudumia waathirika wa mapigano ya Mogadishu

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetangaza kujumuika na shirika la Denmark, lenye kuhudumia wahamiaji (DRC) na pia shirika la kizalendo linalohusika na huduma za amani Usomali, SYPD, kwenye shughuli za kusaidia kaya 6,000, sawa na watu 47,000 walioangamizwa katika eneo la Mogadishu.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu anaamini makosa ya vita yamefanyika Usomali

Kamishan Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, ameripoti Ijumaa kwamba ana ushahidi thabiti wenye kuonyesha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ulifanyika katika mapigano ya karibuni kwenye mji wa Mogadishu, ambapo pia sheria ya kiutu ya kimataifa iliharamishwa kutokana na vitendo ambavyo anavitafsiri kisheria kuwa ni "makosa ya jinai ya vita".

Usomali inazingatiwa tena na Baraza la Usalama

Asubuhi Baraza la Usalama lilikutana kwenye kikao cha hadhara kusailia hali, kijumla, katika Usomali hususan shughuli za kulinda amani za AMISOM.

Kamishna wa Haki za Binadamu ameshtushwa na idadi ya majeruhi na maututi katika Xinjiang

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu amenakiliwa Ijumanne akieleza kuwa ameshtushwa sana na idadi kubwa ya majeruhi na mauaji yaliotukia mwisho wa wiki iliopita, kutokana na fujo zilizofumka katika eneo la Urumqi, mji mkuu wa Jimbo la Uchina Linalojitawala la Xinjiang.

Mapigano ya karibuni Mogadisho yawaong'olesha makazi 200,000 ziada, imeripoti UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti, kwa kupitia msemaji wake aliopo Geneva, kwamba muongezeko wa mapigano yaliovuma karibuni kwenye mji wa Usomali, wa Mogadishu, ni hali iliozusha athari mbaya kabisa kwa wakazi waliolazimika kuhama mastakimu yao, na kuleta usumbufu mkubwa kwa raia wa kawaida.

Mwendesha Mashitaka wa ICC aitaka korti ya rufaa iruhusu kukamatwa raisi wa Sudan

Luis Moreno-Ocampo, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) ameripotiwa kutangaza kwamba ana ushahidi ziada, utakaomwezesha ofisi yake kutoa hati ya kukamatwa kwa Raisi Omar Al-Bashir wa Sudan, kwa madai alihusika na mauaji ya halaiki nchini kwao.

Misri kutangaza itafungua mipaka na Ghaza mara tatu kwa mwezi kuhudumia misaada ya kiutu

Mkuu wa serikali ya utawala wa Tarafa ya Ghaza, anayehusika na masuala ya mipaki, Ghazi Hamad, aliripoti kuwa wenye madaraka Misri wamearifu rasmi kuwa na sera mpya juu ya kivuko cha Rafah, mpakani baina ya Misri na Tarafa ya Ghaza.

Uamuzi wa Tanzania kuongeza muda wa makazi kwa Waburundi wapongezwa na UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limekaribisha uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kuruhusu muda zaidi wa kukaa nchini, kwa baadhi ya wahamiaji wa Burundi 36,000 wanaotaka kurejea makwao, kwa khiyari, kutoka kambi ya Mtabila iliopo wilaya ya Kasulu, kaskazini-magharibi katika Tanzania, kambi ambayo ilipangwa kufungwa mnamo tarehe 30 Juni 2009.

Siku ya Ushikamano wa Kimataifa na Walioathirika Mateso

Tarehe ya leo, 26 Julai, inaadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Ushikamano Kimataifa na Wathirika wa Mateso.